

Lugha Nyingine
Mtu wa kumi aliyekumbwa na ajali ya kuanguka kwa nyumba iliyojengwa na wakazi aokolewa (2)
Mtu wa kumi aliyekwama katika nyumba iliyoanguka ambayo ilijengwa na wakazi wenyewe wa Changsha, katika Mkoa wa Hunan nchini China ameokolewa leo Alhamisi, saa sita usiku, ikiwa ni masaa 132 yamepita tangu ajali hiyo ilipotokea.
Tarehe 29, Aprili, saa sita na dakika 24 mchana, nyumba iliyojengwa na wakazi wenyewe kwenye eneo la Wangcheng, Mji wa Changsha ilianguka. Kwa mjibu wa uchunguzi wa awali, watu 23 walikwama ndani ya nyumba hiyo iliyoanguka, na watu 39 wengine waliokuwa karibu na eneo hilo hawapatikani kwenye mawasiliano. Hadi asubuhi mapema ya leo Tarehe 5, watu watano wamethibitishwa kufariki.
Baada ya mtu wa 10 kuokolewa na kupakiwa kwenye gari la kubeba magonjwa, waokoaji wameendelea kutafuta wengine waliokwamba kwenye kina cha eneo la ajali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma