Ofisa Mkuu wa Hong Kong awaaga wahudumu wa afya wa China Bara waliosaidia mapambano dhidi ya janga la UVIKO-19 (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2022
Ofisa Mkuu wa Hong Kong awaaga wahudumu wa afya wa China Bara waliosaidia mapambano dhidi ya janga la UVIKO-19
Washiriki wa timu ya wahudumu wa afya kutoka China Bara wakiwasilisha vazi maalumu la kujikinga na virusi vya Korona lenye saini zao kwa Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) Carrie Lam (wa tatu kushoto) wakati wa hafla ya kushukuru na kuwaaga. (Xinhua/Li Genge)

HONG KONG - Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) Carrie Lam Alhamisi wiki hii ameagana na kundi la mwisho la timu ya wahudumu wa afya kutoka China Bara inayoondoka Hong Kong wakati wa hafla ya shukrani na kuwaaga iliyoandaliwa na Serikali ya HKSAR.

Ili kuunga mkono mapambano ya Hong Kong dhidi ya wimbi la tano la janga la virusi vya Korona (UVIKO-19), Serikali Kuu ya China na serikali ya mkoa wa Guangdong hapo awali zilituma timu ya wahudumu wa afya kusaidia kutibu wagonjwa wa UVIKO-19 kwa ombi la Serikali ya HKSAR. Timu ya wahudumu wa afya ilijumuisha wataalamu wa afya 391 kutoka taaluma tofauti katika hostapili 25 za China Bara.

Wakati wa uwepo wao huko Hong Kong, wahudumu hao wa afya kutoka China Bara walifanya kazi kwa karibu na wahudumu wa afya kutoka Idara ya Usimamizi wa Hospitali ya Hong Kong ili kuongeza uwezo wa kulaza wagonjwa katika kituo cha matibabu cha jamii kwenye Kituo cha Maonyesho ya Asia na Dunia ndani ya muda mfupi, kuwawezesha wagonjwa zaidi wa UVIKO-19 wanaohitaji kutibiwa wapate matibabu na kuongeza kasi ya jumla ya kutoa huduma kwa wagonjwa wote, ambayo ilisaidia serikali ya HKSAR kutekeleza kikamilifu mkakati wa matibabu.

Katika hotuba yake, Lam ameelezea shukrani za dhati kwa niaba ya HKSAR kwa timu ya wahudumu wa afya kutoka China Bara kwa kujiunga kwenye mstari wa mbele wa kutibu wagonjwa wa UVIKO-19 wakati hali ya janga huko Hong Kong ilipokuwa mbaya zaidi. Amesema anaamini kwamba hivi karibuni Hong Kong itaondokana na janga hilo na amewakaribisha wahudumu hao wa afya kutembelea tena Hong Kong kwa utalii na kuendeleza urafiki na wenzao wa Hong Kong.

He Jing, Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Uhusiano baina ya Serikali ya Hong Kong na Serikali Kuu ya China amesema kuwa timu ya wahudumu wa afya kutoka China Bara imeonyesha kiwango cha juu sana cha utaalamu na kujitolea, na imesifiwa sana na watu wa hali mbalimbali kwenye jamii ya Hong Kong.

Naye kiongozi wa timu ya wahudumu wa afya ya China Bara Chong Yutian amesema kuwa wahudumu wa afya wa timu hiyo wanahisi kutiwa nguvu wanapoona uhai ukirejeshwa huko Hong Kong, na alisema, kwa msaada wa serikali kuu na juhudi za pamoja za watu wote wa Hong Kong, wimbi la tano la janga la UVIKO-19 limetulia.

Siku ya Alhamisi wiki hii, Hong Kong iliandikisha watu 148 walioambukizwa virusi vya korona kufuatia vipimo vya virusi vya Korona vilivyofanywa, na watu wengine 173 walioambukizwa virusi vya korona hivi majuzi kupitia vipimo vya watu kujipima wenyewe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha