Ujenzi wa Hospitali ya kukabiliana na hali ya dharura ya Hongkong na hospitali ya muda ya Lok Ma Chau umekamilika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2022
Ujenzi wa Hospitali ya kukabiliana na hali ya dharura ya Hongkong na hospitali ya muda ya Lok Ma Chau  umekamilika
Muonekano wa halfa ya kukamilika na kukabidhiwa kwa hospitali ya kukabiliana na hali ya dharura ya Hongkong na hospitali ya muda ya mchemraba ya Lok Ma Chau, ambazo zimejengwa kwa msaada wa serikali kuu ya China. (Picha ilipigwa Tarehe 6, Mei.)

Baada ya kufanya kazi ngumu kwa siku 51 mchana na usiku, ujenzi wa hospitali ya kukabiliana na hali ya dharura ya Hongkong na hospitali ya muda ya mchemraba ya Lok Ma Chau umekamilika hivi karibuni. Hafla ya kukamilika na kukabidhiwa kwa hospitali hizo zilizojengwa kwa msaada wa serikali kuu ya China ilifanyika mchana wa Mei 6. Timu maalumu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya korona ya China Bara, Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong, serikali ya Mji wa Shenzhen na watu husika wa Shirika la Ujenzi la China walishiriki kwenye hafla hiyo .  

Ujenzi wa hospitali ya kukabiliana na hali ya dharura ya Hongkong kwa msaada wa serikali kuu ya China ulianzia Machi 6, 2022, na kukamilika na kufanyiwa ukaguzi Aprili 20. Ujenzi wa Hospitali ya muda ya mchemraba ya Lok Ma Chau ulianzia Machi 22 na ulikamilika na kufanyiwa ukaguzi Aprili 25.

(Mpiga picha: Liang Xu/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha