Wanawake wa kijiji cha Kenya wasuka vikapu ili kuongeza kipato (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2022
Wanawake wa kijiji cha Kenya wasuka vikapu ili kuongeza kipato
Wanawake wakisuka vikapu kwenye kijiji cha Katangi cha Machakos, Kenya, Mei 3, 2022. (Picha/Xinhua)

Katika kijiji tulia cha Katangi kilichoko Machakos ya Mashariki ya Nairobi, Kenya, wanawake wengi wanasuka vikapu vya katani chini ya miti.

Kwa wanawake hao, kazi ya kusuka vikapu imekuwa chanzo muhimu cha kupata haki ya kiuchumi, na pia ni sehemu kubwa ya mali yao ya urithi wa kitamaduni.

“Mtindo wa ninavyovaa pamoja na sura yangu vyote vinatokana na kazi hiyo ya kusuka kiondo (kikapu). Hakuna mtu yeyote anayenisaidia,” alisema Peninah Mueni, mwenyekiti wa shirikisho lake la wafumaji vikapu.

Shirikisho la wafumaji vikapu la Mueni lilianzishwa mwaka 2015, likitoka kabila la Wakamba, jamii inayoongea lugha ya Bantu ambayo iko kwenye tambarare pana ya Kusini Masharki mwa Kenya. Katika shirikisho hilo kuna wanawake 30 wenye umri mbalimbali, ambao wanahitaji kupata kipato katika hali yenye nafasi chache za ajari, na elimu yao ni ya kiwango cha chini.

“Ndani ya mwezi mmoja, tunaweza kusuka vikapu 70 vyenye saizi tofauti; kila mmoja wetu anaweza kupata shilingi 15,000 (dola za Marekani 129.38). Baada ya kumaliza oda moja, kipato cha kila mmoja kinategemea kiasi cha vikapu alivyosuka ,” alisema Mueni.

Hivi karibuni oda zao zinatoka Afrika Kusini, ambapo waliuza vikapu vidogo 100. Masoko mengine ya kimataifa waliyoingia ni pamoja na yale ya nchini Ghana na China. Kazi ya wanawake hao imesifiwa na watu, hii imeonesha kufanikiwa kwa mkakati wa wanawake hao wa kuingia soko.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha