China yafaulu kurusha chombo cha kubeba mzigo Tianzhou No.4

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2022
China yafaulu kurusha chombo cha kubeba mzigo Tianzhou No.4

Saa 1:46 alfajiri ya tarehe 10, Mei, Roketi ya Changzheng No.7 iliyobeba chombo cha mzigo Tianzhou No.4 ikarushwa angani, baada ya dakika 10 hivi, chombo na roketi zilifaulu kutengana, na chomo hicho kimeingia vizuri kwenye obiti iliyopangiwa kwenye anga ya juu, saa 2:23, paneli ya mwanga wa jua ilianza kufanya kazi bila tatizo, na kazi hii ya kurusha chombo imepata mafanikio mazuri. Hii ni mara ya kwanza ya kurusha chombo kwenye anga ya juu katika kipindi cha ujenzi wa kituo cha anga ya juu cha China , pia ni safari ndefu ya nne kwa mfumo wa uchukuzi wa mizigo wa kituo cha anga ya juu.

Hadi sasa, pazia la ujenzi wa kituo cha anga ya juu cha China limefunguliwa rasmi na jukumu muhimu la kufikia lengo la kimkakati la hatua tatu la mradi wa China wa kupeleka chombo kinachobeba binadamu kwenye anga ya juu limeanza kutekelezwa.

(Mpiga picha: Guo Cheng/Xinhua) 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha