Lugha Nyingine
Xi awapa moyo vijana kusonga mbele katika safari mpya ya ustawishaji wa taifa
Rais Xi Jinping wa China Jumanne alisema kuadhimisha miaka 100 ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kunalenga kuwapa moyo wanachama wake kusonga mbele katika safari mpya ili kutimiza ndoto ya China ya ustawishaji wa taifa.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, alisema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Umoja wa Vijana wa CPC (CYLC) hapa Beijing.
Taifa linalowapa vijana matumaini makubwa na linalodumisha uhai wa ujana litapata ustawi na neema, alisema Xi.
Katika risala yake, rais Xi alitaja mchango waliutoa wanachama wa Umoja wa Vijana katika miaka 100 iliyopita.
Alipozungumzia matarajio yake kwa Umoja wa Vijana, rais Xi alisema, Umoja wa Vijana unatakiwa kutoa mafunzo kwa vijana kwa ajili ya Chama cha Kikomunisti cha China , na siku zote uwe shule ya kisiasa ya kuongoza vijana kupata maendeleo ya kifikra.
Aliongeza kuwa, Umoja wa Vijana siku zote unatakiwa kuwa nguvu ya utangulizi ya kuwahamasisha vijana wa China wafanye juhudi bila kusita.
Xi Jinping aliutaka Umoja wa Vijana uwe “daraja” yenye nguvu zaidi inayounganisha Chama na vijana wa China tangu mwanzo hadi mwisho, na kujifanyia mageuzi.
Xi alisema, wanachama wa Umoja wa Vijana wanatakiwa kuwa mifano ya kuigwa katika maisha na kazi, kushiriki kwa makini kwenye masomo ya kisiasa, kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kutimiza lengo la fahari la kuwa wanachama wa CPC wanaolingana na matakwa. Na pia aliwahimiza wawe na nia thabiti na kuimarisha ujasiri na ufundi wao wa kupambana na changamoto.
Aliongeza kuwa, wanatakiwa pia kuwa wazalendo na wavumbuzi, wakati huohuo hawataelekezwa njia kwa makosa na hawatakuwa woga mbele ya taabu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma