Miji katika safu za Milima ya Himalaya nchini China yaboreshwa na kuwa ya kisasa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2022
Miji katika safu za Milima ya Himalaya nchini China yaboreshwa na kuwa ya kisasa
Tashi Tsering akipiga ala ya muziki ya kitamaduni ya Tibet katika mkahawa wake wa chai katika Kitongoji cha Rongxar, Kaunti ya Dingri kwenye Mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China, Aprili 10, 2022. (Xinhua/Liu Ying)

LHASA - Baada ya kuweka chupa ya chai, baadhi ya biskuti na filimbi ya harmonica kwenye mkoba wake, Tashi Tsering anavaa sare yake ya kijani, kunywa chai ya maziwa aliyopewa na mke wake, na kuelekea kwenye lori lake kuanza kazi za siku katika eneo la ndani la safu za Milima ya Himalaya.

Tashi Tsering, 45, ni mlinzi wa doria huko Rongxar, mji wa mpakani katika Kaunti ya Dingri, kwenye Mkoa unaojiendesha wa Tibet nchini China.

Majukumu ya Tashi Tsering na wenzake yanahusisha kutunza mabango na kukusanya taka katika Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Mlima Qomolangma. Makundi ya kondoo-mwitu mara nyingi hupita wakati wakipiga doria.

"Zamani wanyama pori walikuwa wanakimbia wakiona binadamu, kwa sasa wanatujia bila woga," anasema Tashi Tsering.

Mnamo Aprili 2015, mji huo wenye wakazi 1,000, uliathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katika nchi jirani ya Nepal, na nyumba nyingi zilibomolewa.

Kufuatia tetemeko hilo la ardhi, serikali inawekeza sana katika ujenzi mpya. Kwa miaka mingi, nyumba zilizojengwa kwa chuma na barabara za saruji zilijengwa, na mawimbi ya mawasiliano ya simu yapatikana na hivyo mtandao wa simu unapatikana kwa kiwango kikubwa.

"Sasa, vijana wanafanya ununuzi mtandaoni. Watu wamevaa kila aina ya viatu vya ngozi, raba na viatu vya kupanda mlima," Dawa Norbu mkazi wa kijiji hicho anasema, akiongeza kuwa magari ya kubebea mizigo huja mjini humo mara kwa mara.

Usafiri bora pia huleta watalii wengi zaidi, wanaokuja kuona mahali pa faragha na mandhari ya kupendeza.

Kando na kufanya kazi ya ulinzi wa doria, Tashi Tsering pia anaendesha mkahawa wa chai ya maziwa. Mwaka jana, alikarabati vyumba vitatu vya wageni vya nyumba yake na kuanza kutoa huduma ya malazi kwa watalii.

"Nyumba ya chai na makazi pekee huniingizia kipato cha zaidi ya yuan 400,000 (kama dola za Kimarekani 61,000) kwa mwaka," anasema Tashi Tsering, na kuongeza kuwa yeye pia anapenda kupiga filimbi ya harmonica na ala nyingine kwa wageni wake kwenye mkahawa wake wa chai anaporudi kutoka doria.

Mwaka jana, mapato ya kila mtu ya mji huo yaliongezeka kwa asilimia 14 hadi kufikia zaidi ya yuan 15,800, sehemu kubwa ya faida hiyo ilitokana na shughuli za utalii zinazoshamiri kwa wingi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha