Juhudi za Familia ya Sherpa za kuhifadhi ngoma ya jadi chini ya Mlima Qomolangma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2022
Juhudi za Familia ya Sherpa za kuhifadhi ngoma ya jadi chini ya Mlima Qomolangma
Picha iliyopigwa Aprili 13, 2022 ikionesha Tarafa ya Zhentang, ambayo inazungukwa na misitu asilia chini ya Mlima Qomolangma ndani ya Milima ya Himalaya, Wilaya ya Dinggye ya Xigaze ya Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini Magharibi mwa China, Aprili 13, 2022. (Picha/Xinhua)

Ingawa mjukuu wake wa kike ana umri wa miezi saba tu, Namkha mwenye umri wa miaka 57 anapenda kucheza ngoma mbele ya mjukuu wake huyo, akimuonesha baadhi ya vitendo vya ngoma ya jadi ya Sherpa.

“Mwanafunzi wangu mwenye umri wa miaka zaidi ya 40 ambaye ni mwenye miaka mingi zaidi kuliko wanafunzi wangu wengine, na aliye mdogo zaidi ni mjukuu wangu wa kike,” alisema huyu Msherpa akiwa na tabasamu kwenye uso wake. Anatarajia mjukuu wake wa kike atarithisha ngoma ya jadi siku za baadaye kama yeye.

Namkha anaishi katika Tarafa ya Zhentang ya Wilaya ya Dinggye ya Mkoa unaojiendesha wa Tibet, Kusini Magharibi mwa China, akiwa mrithi wa ngoma ya Sherpa ya Zhentang, ambayo ni mali ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usiogusika.

Kutokana na uungaji mkono wa serikali, kila kijiji huko kimeanzisha kikundi cha maonesho ya ngoma chenye watu 16 kwa wastani. Serikali hiyo pia ilitenga fedha kwa kujenga kituo cha maonesho ambapo watu wanaweza kucheza ngoma.

Hivi sasa Namkha amekuwa na wanafunzi 10, watatu wana umri wa zaidi ya miaka 40, wanne wenye miaka zaidi ya 30 na watatu wenye miaka zaidi ya 20. Anapanga kuwafundisha watu wengi zaidi.

“Vijana wengi zaidi wanatakiwa kujiunga nasi na kufanya juhudi za kurithisha ngoma za jadi kizazi hadi kizazi,” alisema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha