Semina kuhusu Sanaa ya Mapango ya Dunhuang yafanika kwa kupitia video

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2022
Semina kuhusu Sanaa ya Mapango ya Dunhuang yafanika kwa kupitia video
Semina kuhusu sanaa ya mapango ya Mogao ya Dunhuang inayoitwa “Utamaduni wa Dunhuang Unaoelekea Ofisi za Ubalozi wa China Duniani --Ubalozi mdogo wa China wa Hamburg” ilifanyika kwa kupitia video. (Picha/Yan Wenhao)

Semina kuhusu sanaa ya mapango ya Mogao ya Dunhuang iliyoitwa “Utamaduni wa Dunhuang unaoeleka Ofisi za Ubalozi – Ubalozi mdogo wa China wa Hamburg” ilifanyika kwa kupitia video mchana wa Mei 15, 2022.

Wang Wei, konsela mkuu wa ubalozi mdogo wa China huko Hamburg, kwenye hotuba yake ya semina alieleza kuwa, watafiti wanaojikitia katika utafiti wa Dunhuang wametoa mchango kwa ajili ya mambo haya, wakifanya juhudi za utafiti zisizolegea hata kidogo juu ya utamaduni wa Dunhuang, na kuendana na wakati na kujitahidi kuvumbua njia mpya, ili kuifanya dunia kufahamishwa vizuri zaidi utamaduni wa Dunhuang.

Mji wa Hamburg ulikuwa na mawasiliano na China kwa muda mrefu kuanzia karne ya 18. Hivi sasa, Hamburg bado ni kituo muhimu cha mawasiliano kwenye nchi kavu na bahari kwenye “Ukanda mmoja, Njia moja”, na inafanya kazi muhimi katika kusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Ujerumani na ya China na Ulaya.

Mwaka 2022 ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia wa China na Ujerumani. Semina hiyo iliandaliwa pamoja na Ofisi ya mambo ya nje ya serikali ya Mkoa wa Gansu, Taasisi ya Dunhuang na serikali ya mji wa Dunhuang, na ina umuhimu mkubwa kwa wakati huu maalumu.

Semina hiyo inatarajia kuwafanya watu wengi zaidi kupenda utamaduni wa Dunhuang. Baada ya kuisha kwa maambukizi ya virusi vya korona, nchi hizo mbili zitaimarisha mabadilishano zaidi, kufanya kazi pamoja ili kueneza utamaduni wa Dunhuang kwa dunia nzima, kugundua zaidi misingi ya utamaduni wa Dunhuang, na kujenga mawasiliano ya karibu zaidi kati ya watu.

Ma Cong, mjumbe wa kikundi cha viongozi wanachama wa CPC na naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya serikali ya Mkoa wa Dunhuang alisema, anatumai kwa kupitia semina hiyo, wafanyakazi wa ofisi za ubalozi wa China katika nchi mbalimbali na Wachina wanaoishi nchi za nje wanaweza kuongeza uelewa wao kuhusu utamaduni wa Dunghuang na Njia ya Hariri. Na pia anatumai semina hii itakuwa fursa ya kukutana na marafiki wengi zaidi wanaounga mkono utamaduni wa Dunhuang.

Bw. Ma alisema, ofisi ya mambo ya nje ya serikali ya Mkoa wa Gansu itasimulia kwa bidii zaidi hadithi ya Dunhuang, hadithi ya Gansu na hadithi ya China.

Katibu wa Kamati ya Chama ya Chuo cha Dunhuang Zhao Shengliang alifanya mhadhara kuhusu sanaa ya mapango ya Dunhuang kwa kupitia video, akijulisha kazi za kufukuliwa kwa mapngo, mitindo ya mapango, sifa za sanamu zenye rangi mbalimbali, mada za picha kwenye ukuta na mafanikio yake ya kisanaa na ujuzi mwingine muhimu kadha wa kadha. Na pia alijulisha juhudi na mafanikio ya chuo hicho katika kulinda, kusoma na kuendeleza utamaduni wa Dunhuang.

Naibu Katibu wa kamati ya Chama ya Mji wa Dunhuang Wang Jin pamoja na watu wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Mkoa wa Gansu, Chuo cha a Dunhuang, serikali ya Mji wa Dunhuang walihudhuria semina hii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha