Waziri Mkuu wa China asisitiza utekelezaji wa haraka wa sera kuu za uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2022
Waziri Mkuu wa China asisitiza utekelezaji wa haraka wa sera kuu za uchumi
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, akiongoza kongamano la kuleta utulivu wa ukuaji wa uchumi, lililofanyika katika Mkoa wa Yunnan Kusini Magharibi mwa China, Mei 18, 2022. (Xinhua/Rao Aimin)

KUNMING - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang ametoa wito wa kuharakishwa kwa kasi na kuongeza juhudi katika utekelezaji wa sera kuu za uchumi.

Li, ambaye pia mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, aliyasema hayo alipoongoza kongamano la kuleta utulivu wa ukuaji wa uchumi, lililofanyika katika Mkoa wa Yunnan nchini China Jumatano wiki hii.

Amesisitiza kufanya juhudi za kuleta utulivu katika ukuaji wa uchumi ili uwe mhimili thabiti, kuweka mkazo katika maendeleo tulivu ya wadau wa soko, ili yawe mtegemezi thabiti kwa nafasi za ajira na maisha ya kimsingi ya watu.

Akiweka wazi kuwa wimbi jipya la kuibuka tena kwa UVIKO-19 nchini China na mabadiliko katika hali ya kimataifa yamesababisha shinikizo zaidi kwa uchumi, Li amesisitiza umuhimu wa kujiamini, akisema, nchini China kuna wadau wa soko wa China zaidi ya milioni 150, ambapo kuna ustahimilivu mkubwa, na bei thabiti kwa ujumla.

"Siku zote tumesisitiza kuepuka vichocheo vya uchumi ambavyo 'ni kama mafuriko'. Hatukutoa vichocheo vya kifedha, hata wakati UVIKO-19 ulipotuathiri zaidi Mwaka 2020," Li amesema, na kuongeza kuwa bado kuna nafasi ya kuboresha sera nchini ili kukabiliana na changamoto mpya.

Amesisitiza umuhimu wa juhudi za kuratibu udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Korona na maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa njia yenye ufanisi zaidi, na umuhimu wa kuimarisha udhibiti na marekebisho kwa ujumla.

Sera nyingi zilizotolewa kwenyeMkutano wa Serikali Kuu wa Kazi za Kiuchumi na ripoti ya kazi ya serikali zilitekelezwa katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2022, Li ametoa wito kwa serikali za mitaa kuweka hatua zaidi katika Mwezi Mei, ili kuufanya uchumi urudi haraka kwenye hali ya kawaida

“Nchi lazima ihakikishe utekelezaji kamili wa hatua zake za unafuu wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupunguzwa kwa kodi na marejesho ya kodi, ili makampuni ya biashara yaweze kufurahia msaada wa sera kwa wakati na kikamilifu” Li amesema.

Kuhusu kuleta utulivu wa uchumi, Li amesema kwamba China lazima ihakikishe utoaji wa kutosha wa nafaka na nishati, na kudumisha utulivu wa bei za vitu na mambo yote yanayochangia maendeleo ya kiuchumi.

Li pia amesema kwamba, China itahimiza kuorodheshwa kwa kampuni zinazojihusisha na uchumi wa kidijitali na majukwaa ya mtandaoni katika masoko ya hisa ndani na nje ya nchi kwa mujibu wa sheria na kanuni, na kutunga sheria na kuweka mazingira ya biashara ambayo ni ya uwazi, usawa na yenye mwelekeo wa uvumbuzi.

Maofisa wa serikali kutoka mikoa 12 ya Mashariki, Kati, Magharibi na Kaskazini Mashariki mwa China walihudhuria kongamano hilo. Mikoa 10 kati ya 12 hiyo inachukua nafasi 10 za mbele kwenye orodha ya mikoa bora inayochangia uchumi wa jumla wa China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha