WHO yaahidi kuisaidia Tanzania kwa nguvu zote kuanzisha udungaji wa chanjo ya polio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2022
WHO yaahidi kuisaidia Tanzania kwa nguvu zote kuanzisha udungaji wa chanjo ya polio
Watoto wakisubiri kudungwa chanjo ya polio huko Dar es Salaam, Tanzania Mei 18, Mwaka 2022. (Mpiga picha: Herman Emmanuel/Xinhua)

Jumatano Tanzania imeanzisha duru ya pili ya udungaji wa chanjo ya polio, na Shirika la Afya Duniani (WHO) liliahidi kutoa msaada wa kiufundi na utaratibu kwa shughuli ya udungaji wa chanjo hiyo.

Shirika la Afya Duniani lilisema kwenye taarifa kuwa litatoa msaada wa kiufundi pamoja na UNICEF na Pendekezo la Kutokomeza ugonjwa wa Polio duniani.

Taarifa hiyo ilisema kampeni kubwa ya chanjo ya nyongeza imeanzishwa kutoka Mei 18 hadi Mei 21 katika wilaya 195 nchini Tanzania na itawanufaisha watoto 10,576,805 wenye umri chini ya miaka 5.

Duru ya kwanza ya kampeni ya udungaji wa chanjo hiyo ilifanyika kuanzia Machi 24 hadi Machi 27 na kuwafikia watoto zaidi ya milioni 1 katika mikoa minne ya Mbeya, Njombe, Ruvuma na Songwe inayopakana na Malawi baada ya nchi hiyo kuripoti mlipuko wa maambukizi ya virusi vya polio .

Mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Zabulon Yoti alisema, “kampeni hii ni hatua muhimu ya kudhibiti maambukizi ya virusi kwa Tanzania ili kuwafanya watoto wote wanaofaa kudungwa chanjo ya polio,”Aliongeza kuwa tunashukuru Pendekezo la Kutokomeza ugonjwa wa Polio Duniani na watu wanaochangia kampeni hiyo, hii ni kazi muhimu kwa kudumisha hali isiyo na ugonjwa wa polio nchini Tanzania.

Taarifa hiyo ilisema, Malawi ilitangaza mlipuko wa maambukizi ya virusi vya polio Februari 17 baada ya kugunduliwa kwa mtoto mmoja aliyepatwa na ugonjwa.

Taarifa ilisema kuwa, ingawa nchi ya Tanzania imeanzisha mfumo nyeti wa kufuatilia ugonjwa wa polio, lakini ilithibitishwa kuwa nchi isiyo na ugonjwa wa polio mwaka 2015 baada ya miaka mingi bila kugunduliwa kwa wagonjwa wa polio. Iliongeza kuwa kutokana na udungaji wa chanjo kwa watu wengi, nchini Tanzania haijagunguliwa hata kwa mtoto mmoja aliyepatwa na ugonjwa wa polio tokea Mwaka 1996. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha