Shughuli ya kuonesha nafasi za ajira ya Kampuni za China nchini Misri yavutia wahitimu wa vyuo vikuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2022
Shughuli ya kuonesha nafasi za ajira ya Kampuni za China nchini Misri yavutia wahitimu wa vyuo vikuu
Mwanafunzi wa Misri akijaza fomu kwenye kibanda cha kampuni ya China wakati wa shughuli ya kuonesha nafasi za ajira ya kampuni za China nchini Misri huko Ismailia, Misri, Mei 17, 2022. (Picha/Xinhua)

Shughuli ya kuonesha nafasi za ajira ya kampuni za China katika Misri ilifanyika tena Jumanne katika mji wa Kaskazini Mashariki mwa Misri baada ya kukatika kwa miaka miwili kwa sababu ya UVIKO-19, ikionesha mamia ya nafasi za ajira kwa wanafunzi wenye matarajio waliohitimu kutoka vyuo vikuu.

Kampuni za China zaidi ya 25 nchini Misri zilishiriki kwenye shughuli hiyo iliyofanywa na Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Mfereji Suez na Baraza la Biashara la Misri-China, zikihusisha kampuni za ujenzi, mawasiliano ya habari, ufumaji nguo, usambazaji wa bidhaa na ufugaji.

“Nilijaza fomu nyingi za maombi ya ajira na kwenda kufanywa usaili na kampuni tatu za China,” alisema Mariam Roushdy, mwanafunzi wa mwaka wa nne wa Chuo Kikuu cha Mfereji Suez anayesoma somo la lugha ya Kichina, wakati alipohojiwa na Shirika la Habari la Xinhua.

“Shughuli hiyo inaokoa nafasi yangu ya muda na nguvu yangu, kwa kuwa tunakutana na waajiri wengi kwenye sehemu moja badala ya kusafiri mpaka mikoa kadhaa. Na kwenye shughuli ya mwaka huu kuna nafasi mbalimbali za kazi ya mkalimani, ajira kwenye miradi na uhasibu,” alisema huyu anayeonekana kuwa na uwezo wa kufanya kazi ya mkalimani.

Mamia ya wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu walioandaa CV walikusanyika kwenye shughuli hiyo na kutarajia kupata kazi ya kufanya mazoezi au ya kudumu. Na kampuni kutoka sehemu mbalimbali za Misri pia zilishiriki kwenye shughuli hiyo, zikiwemo eneo la uchumi la Mfereji Suez, Mji Mkuu mpya wa usimamizi, mji wa Mediterrania New Alamein na Mji Mkuu Cairo.

Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang aliamini kuwa, kampuni za China “zitaleta nafasi nyingi zaidi kwa watu wa Misri kutokana na kuendelea kwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.”

Balozi huyo alisema, anaamini kampuni za China nchini Misri zinajitahidi kufanya maendeleo ya China yataleta fursa kwa ajili ya Misri kuendelea kupata maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha