Ghala pekee ya China ya mbegu za mazao ya sehemu za baridi yakamilisha upanuzi wake mkoani Heilongjiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2022
Ghala pekee ya China ya mbegu za mazao ya sehemu za baridi yakamilisha upanuzi wake mkoani Heilongjiang
Mfanyakazi akibeba masanduku ya mbegu kwenye ghala ya mbegu za mazao ya sehemu za baridi iliyoko Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Mei 19, 2022.(Picha/Xinhua)

Upanuzi wa ghala hiyo pekee ya China ya mbegu za mazao ya sehemu za baridi umekamilika hivi karibuni kwa ajili ya kuinua uwezo wake wa kuhifadhi sampuli za mbegu 80,000 hadi 200,000.

Ghala hiyo ya mbegu iko katika Mkoa wa Heilongjiang wa Kaskazini zaidi mwa China, imehifadhi sampuli zaidi ya 50,000 za mbegu za mazao mbalimbali. Sampuli zaidi ya 2,000 za soya porini, ambayo ni mmeapori wa daraja la pili unaohifadhiwa nchini China, sasa zimehifadhiwa kwenye ghala hiyo, na mbegu za soya ya aina hii zinachukua asilimia 25 ya zile za ujumla nchini China. (Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha