

Lugha Nyingine
Kijana wa Kenya aliyeandaliwa kwa msaada wa China amekuwa dereva mstadi wa treni ya kisasa (3)
![]() |
John Pius (Kulia) na Brian Kemboi wakihakikisha usalama kwa wafanyakazi kwenye jukwaa huko Kajiado, Kenya, Machi 25, 2022. (Picha/Xinhua) |
John Pius alizaliwa na kukua kwenye kijiji cha Kusini Mashariki mwa Kenya, ambapo reli ya upana wa mita moja yenye historia ya miaka 100 imepita, na alishangaa kuona treni kupanda mteremko na kwenda kwa mbali.
Mnamo Mwezi Februari, Pius alijiunga na madereva wa kwanza wa treni wa Kenya, na siku zote anaendesha treni ya abiria kwenye reli ya SGR inayokwenda Nairobi hadi Suswa yenye urefu wa kilomita 120, ambayo ilizinduliwa Oktoba 16, 2019.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 32 alisoma somo la uhandisi wa mashine, alianza kusoma kwenye darasa la muda mfupi la udererva wa treni mwaka 2016, na mwaka mmoja baadaye, reli ya SGR ya Nairobi-Mombasa yenye urefu wa kilomita 48 iliyojengwa kwa msaada wa China ilizinduliwa. Pius alipata mafunzo ya mtaalam kutoka China, ambaye alimfundisha ujuzi wa kimsingi kuhusu kuendesha treni ya abiria ya kisasa, ukiwa ni sehemu ya juhudi za kuhimiza uhamishaji wa teknolojia na ufundi wa kazi kati ya China na Kenya.
“Tokea mwaka 2016 nikiwa nimefanya kazi pamoja na mwalimu wa China, na nimepata ufundi unaotumika sana, kama vile kuendesha treni , kushughulikia matatizo, na namna ya kuanzisha mawasiliano na watu wengine,” alisema Pius.
Pius alisema, hadi sasa, wapo madereva 10 wenye uwezo wa kuendesha treni kwenye reli ya SGR ya Nairobi-Mombasa, na madereva hao waligawanywa kwa wastani katika kazi za kusafirisha abiria na mizigo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma