Mwanafunzi kutoka Zimbabwe afurahia uhuru na shirikishi huko Xinjiang (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2022
Mwanafunzi kutoka Zimbabwe afurahia uhuru na shirikishi huko Xinjiang
Mwanafunzi kutoka Zimbabwe George Tabengwa akitafuta vitabu katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Matibabu cha Xinjiang huko Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, Mei 18, 2022. (Picha/Xinhua)

George Tabengwa, mwanafunzi kutoka Zimbabwe anasoma somo la matibabu kwa miaka minne kwenye Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, Magharibi Kaskazini mwa China, ambapo jambo moja halijabadilika kutoka mwanzo hadi mwisho.

“ Kumbukumbu ya kwanza niliyopata kuhusu Xinjiang, ambayo pia ni taswira ambayo siku zote niliyoiwaza akilini mwangu ni kama hiyo: Xinjiang ni sehemu yenye usalama, uhuru, uzuri na shirikishi,” alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 24.

Tabengwa akiwa mwanafunzi wa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Matibabu cha Xinjiang, alijaaliwa na mkoa huo kuanzia mwaka 2018, ambapo alimaliza masomo ya maandalizi kwenye mkoa wa Shandong, akapata udhamili wa masomo wa kusoma somo la matibabu kwenye chuo hicho.

Licha ya kupata baadhi ya habari potofu kutoka vyombo vya habari vya nchi za Magharibi, alijua mambo machache sana kuhusu Xinjiang. “Baada ya kuja hapa Xinjiang, nimetambua habari zile si kweli,” alisema.

“Sijaona matatizo yoyote, hapa ni salama sana. Kila mmoja anaweza kufanya kazi au mambo kwa anavyopenda,” alisema Tabengwa. “Na mimi pia ninafurahia sana masomo na maisha ya hapa, yakiwemo utamaduni wa aina mbalimbali na upatikanaji rahisi wa chakula mbalimbali.”

 Mvuto mmoja wa sehemu hiyo kwa wanafunzi ni makabila mbalimbali na utamaduni tofauti.

“Wenzetu wanatoka makabila mbalimbali ya China. Wananifundisha lahaja zao mara kwa mara, tunafurahia kucheza pamoja,” alisema Tabengwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha