Miaka kumi ya shule ya eneo la milimani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2022
Miaka kumi ya shule ya eneo la milimani
Mei 30, 2012, watoto wa Shule ya Msingi ya Yudong wakicheza katika barabara ya kupitisha kijijini mbele ya mlango wa shule hiyo. Wakati huo, barabara hiyo ilikuwa ya mchanga na kokoto.

Shule ya Msingi ya Yudong katika Kijiji cha Longfu cha Wilaya inayojiendesha ya kabila la wamiao ya Du’an, Guangxi, ilianzishwa mwaka 1964 ambayo iko katika eneo la Milima ya Dashi lenye hali mbaya ya mazingira ya asili. Mwezi Mei, Mwaka 2012, waandishi wa habari walikuja Shule ya Msingi ya Yudong kwa mara ya kwanza, majengo ya shule hiyo yalikuwa ya hali duni sana, yalikuwa majengo mawili yaliyojengwa zamani sana. Wakati huo, kulikuwa na njia chache tu za mchanga na kokoto katika vijiji zaidi ya 20 katika Kijiji cha Yudong, na wanafunzi wengi walikuwa wakifika shuleni kwa muda wa saa moja au mbili baada ya kupanda milima.

Katika miaka kumi iliyopita, katika kazi za kuwasaidia watoto wa familia zenye hali ya umaskini kwenda shuleni na kustawisha kazi ya elimu, eneo hilo limetenga fedha nyingi kujenga upya na kupanua Shule ya Msingi ya Yudong, sasa shule hiyo imekuwa na majengo mapya ya masomo, majengo ya mabweni, kiwanja cha mpira wa vikapu, bwalo, misalani n.k. Shule hiyo imekuwa na sura mpya, eneo la shule limepanuka kwa mara moja, na hali ya kusoma imeboreshwa sana. Shule hiyo pia imeanzishwa darasa la masomo kupitia mtandao wa internet, darasa la muziki, maktaba, pamoja na mfumo wa kutoa mafunzo kwa kupitia mtandao wa internet ili watoto waweze kupata mengi kuhusu hali ya nje ya eneo la milimani. Zaidi ya hayo, Kijiji cha Yudong, sio tu barabara kuu inapita kijiji hiki, , bali pia kuna barabara ya ngazi ya pili inayopita katikati ya kijiji , hivyo watoto wao wamepata urahisi wa kwenda nje ya mlima.(Mpiga picha:Huang Xiaobang/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha