Shughuli za Mbio ya Mashindano ya Mchezo wa Ngalawa za Dragon kati ya China Bara na Taiwan Zafanyika (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2022
Shughuli za Mbio ya Mashindano ya Mchezo wa Ngalawa za Dragon kati ya China Bara na Taiwan Zafanyika
Tarehe 30, Mei, timu ya ngalawa ya dragon kutoka Chuo Kikuu cha Jimei inafanya mazoezi kwenye Kituo cha Michezo ya Maji ya Xiamen. (Picha/Xinhua)

Wakati sikukuu ya Tarehe 5 ya Mwezi wa 5 kwa kalenda ya kilimo ya China ambayo pia iliitwa kuwa siku ya mashindano ya mchezo wa ngalawa za dragon ya China inapowadai, mashindano ya mbio ya ngalawa za dragon kati ya China Bara na Taiwan ya mwaka 2022 yatafanyika kutoka tarehe 2 hadi 3, Juni huko Xiamen, Mkoa wa Fujian, China.

Mashindano ya mbio ya ngalawa za dragon ikiwa shughuli ya jadi ya China yenye historia ndefu, inapendwa sana na watu wa pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan. Habari zinasema, mbio ya ngalawa za dragon ikiwa kiini cha shughuli za mwaka huu, itaanzia tarehe 2, Juni kwenye Ziwa la Ngalawa za Dragon la eneo la Jimei la Mji wa Xiamen. Timu 41 kutoka pande mbili zitashindana pamoja kwenye mchezo huo, zikiwemo timu 24 kutoka China bara na timu 17 kutoka Taiwan. Mbio itagawanywa katika sehemu mbili ya mbio ya mita 300 na mbio ya kuvutana kwa ngalawa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha