Watu 4 wafariki, wengine 14 kujeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi kutokea Sichuan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 02, 2022
Watu 4 wafariki, wengine 14 kujeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi kutokea Sichuan, China
Picha iliyopigwa Juni 1, 2022 ikionesha ndani ya ofisi ya posta iliyoharibika baada ya tetemeko la ardhi huko Baoxing, Mji wa Ya’an wa Mkoa wa Sichuan wa Kusini Magharibi mwa China. (Picha/Xinhua)

Habari kutoka Makao makuu ya uongozi wa kazi ya uokozi baada ya maafa zilisema, watu wanne walifariki na wengine 14 walijeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi kutokea huko Ya’an, Mkoa wa Sichuan wa Kusini Magharibi mwa China.

Habari zilizotolewa na Kituo cha Mtandao wa Tetemeko la Ardhi cha China (CNES) zilisema, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.1 kwenye vipimo vya Richter lilitokea katika Wilaya ya Lushan, Mji wa Ya’an wa Mkoa wa Sichuan Jumatano wiki hii saa 11 mchana kwa saa za Beijing.

Na tetemeko la ardhi lingine lenye ukubwa wa 4.5 kwenye vipimo vya Richter lilitokea baadaye katika Wilaya ya Baoxing ya Mji wa Ya’an Jamatano wiki hii saa 11 na dakika 3 mchana.

Mji wa Ya’an umeanzisha mfumo wa ngazi ya pili wa kukabiliana na hali ya dharura ya tetemeko la ardhi, huku ukikadiria hasara kwenye maafa hayo.

Wahudumu zaidi ya 4500 kutoka idara za uokozi wa dharura, askari polisi, zimamoto, matibabu walipelekwa kwa eneo la tetemeko la ardhi ili kutafuta watu waliojeruhiwa , kukarabati barabara, na kuhamisha watu walioathiriwa na maafa.

Idara ya tetemeko la ardhi ya mkoa huo ilisema, tetemeko la ardhi la Lushan lenye ukubwa wa 6.1 kwenye vipimo vya Richter ni tetemeko linalofuata tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 kwenye vipimo vya Richter, ambalo lilishambulia wilaya hiyo mwaka 2013.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha