

Lugha Nyingine
Zambia yazindua mitambo ya kusaga nafaka iliyotolewa msaada na China (3)
![]() |
Picha iliyopigwa Juni 2, 2022 ikionyesha kiwanda cha kusaga nafaka kilichofadhiliwa na China huko Lusaka, Zambia. (Xinhua/Zhang Yuliang) |
Lusaka – Siku ya Ijumaa mwishoni mwa wiki iliopita Zambia ilizindua rasmi mitambo mitatu ya kisasa ya kusaga nafaka iliyofadhiliwa na China.
Mitambo mitatu ya kiwanda hicho cha kusaga nafaka, yenye uwezo wa kuzalisha tani 520 za unga kwa siku, inatarajiwa kuimarisha usalama wa chakula na kupunguza bei ya unga unaotumika kuandaa chakula kikuu nchini humo.
Hafla ya kuzindua kiwanda hicho ilihudhuriwa na Du Xiaohui, Balozi wa China nchini Zambia na Ambrose Lufuma, Waziri wa Ulinzi wa Zambia.
Katika hotuba yake, mjumbe huyo wa China alisema kuanzishwa kwa mradi huo ni hatua nyingine muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.
Alisema mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha usalama wa chakula na kuleta utulivu wa bei ya unga wa mahindi nchini humo.
Kwa upande wake, Waziri Lufuma alitoa shukrani kwa China kutoa msaada huo, akisema utasaidia sana siyo tu kuongeza uzalishaji kwenye shughuli za kilimo lakini pia kupunguza bei ya unga wa mahindi.
Lufuma alisema Zambia itaishukuru China milele kwa uungaji mkono wake kwa miaka mingi, na kuongeza kuwa China imekuwa mshirika mwenzi wa kuaminika na iko tayari kuunga mkono inapohitajika.
Kwa mujibu wa waziri huyo, mradi huo haujatoa tu ajira wakati wa ujenzi wake bali pia takriban ajira 300 za ziada zimetolewa na mradi huo huku wenyeji wakipewa ujuzi wa kiufundi wa jinsi ya kuendesha mitambo hiyo ya kusaga nafaka.
Mradi huo upo chini ya Mpango wa Rais wa Mitambo ya Kusaga Nafaka. Hapo awali, zaidi ya mitambo 1,000 ya kusaga inayotumia nishati ya jua imefungwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo tangu Mwaka 2015.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma