Mkoa wa Zhejiang nchini China wafanya jitihada za kufikia ustawi wa pamoja wa watu wote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 10, 2022
Mkoa wa Zhejiang nchini China wafanya jitihada za kufikia ustawi wa pamoja wa watu wote
Wanafunzi wa shule ya msingi wakipiga picha baada ya mafunzo ya kuteleza kwenye theluji katika Eneo la Anji, Mkoa wa Zhejiang nchini China, Januari 9, 2022.

Mnamo Juni 2021, Serikali Kuu ya China ilitoa mwongozo wa kujenga Zhejiang kuwa kielelezo au mfano kwa ajili ya kufikia ustawi wa pamoja wa watu wote wa China. Chini ya mwongozo huo, mkoa huo sasa utajitahidi kufikia ustawi wa pamoja wa watu wake ifikapo Mwaka 2035, na pato lake la ndani kwa kila mtu na mapato ya wakaazi wa mijini na vijijini kufikia kiwango cha nchi zilizoendelea.

Ikiwa ni mkoa wenye nguvu ya kiuchumi Mashariki mwa China, Mkoa wa Zhejiang umetayarisha mipango ya kina ili kufikia ustawi wa pamoja wa watu wote. Kwa mujibu wa makadirio, malipo ya wafanyakazi yatachangia zaidi ya asilimia 50 ya Pato la Mkoa (GDP) ifikapo Mwaka 2025, na uwiano wa mapato kwa ajili ya matumizi au akiba ya kila mtu kwa Pato la Mkoa (GDP) yameendelea kuongezeka katika kipindi hicho.

Mkoa huo sasa utaanza kutafuta mafanikio ya kujenga mfumo wa kiwango cha juu wa ajira na ujasiriamali, kuongeza ubora wa utaratibu wa uhakikisho wa kijamii, kukuza ugavi wa huduma bora za umma, na kulenga kufikia ustawi wa pamoja wa watu wote katika maisha ya kiroho. (Xinhua/Huang Zongzhi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha