Mashimo sita ya utambikaji yagunduliwa kwenye Sanxingdui na kufukuliwa kwa mabaki ya kale karibu 13000

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 14, 2022
Mashimo sita ya utambikaji yagunduliwa kwenye Sanxingdui na kufukuliwa kwa mabaki ya kale karibu 13000

Juni 13, Taasisi ya Utafiti wa Mabaki ya Kale ya Mkoa wa Sichuan ilitangaza matokeo mapya kabisa ya utafiti kwenye magofu ya kale ya Sanxingdui katika Mji wa Guanghan, Mkoa wa Sichuan, kuwa mabaki ya kale ya utamaduni karibu 13000 yenye nambari yalifukuliwa kwenye mashimo sita ya utambikaji. Mabaki kadhaa ya kale yenye thamani ambayo maumbo yao ya ajabu ya kipekee hayajaonekana hapo kabla.

Magofu ya kale ya Sanxingdui yako Mji wa Guanghan, Mkoa wa Sichuan, eneo la magofu hayo ni la kilomita 12 hivi za mraba, na yaligunduliwa kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1920 ya Karne ya 20. Tokea mwaka 2020, Timu ya Utafiti wa pamoja wa Mabaki ya kale ambayo iliundwa na taasisi ya utafiti wa kisayansi na vyuo vikuu vikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Mabaki ya Kale ya Mkoa wa Sichuan, Chuo Kikuu cha Beijing, na Chuo Kikuu cha Sichuan, iligundua na kufukulia kwa mfululizo mashimo sita ya utambikaji ya nambari ya 3 hadi 8 yenye historia ya miaka 3000 hivi karibu na mashimo ya utambikaji ya nambari ya 1 na 2. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha