Majibu ya Barua ya Rais Xi Jinping yawatia moyo makada vijana wa vyama sita vya Kusini mwa Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2022
Majibu ya Barua ya Rais Xi Jinping yawatia moyo makada vijana wa vyama sita vya Kusini mwa Afrika
Picha iliyopigwa Juni 10 ikionesha majengo ya Shule ya Uongozi ya Nyerere huko Pwani, Tanzania. (Picha/Xinhua)

Wanafunzi wote wa semina ya makada vijana ya vyama sita vya kusini mwa Afrika ya Shule ya Uongozi ya Nyerere siku hizi walipokea majibu ya burua ya rais Xi Jinping wa China. Barua hiyo iliwafurahisha na kuwatia moyo. Walisema sisi vijana tutatoa nguvu zetu kwa ajili ya maendeleo na ustawishaji wa taifa na ushirikiano kati ya Afrika na China.

“Tunafurahi sana kusoma majibu ya barua ya rais Xi,” alisema Nawanda Yahya, kiongozi wa upande wa Tanzania wa semina hiyo, ambaye pia ni kada wa CCM wa Tanzania, “ingawa rais Xi ana shughuli nyingi, alijibu barua yetu ndani ya wiki moja, hali hii imedhihirisha kuwa anatilia maanani uhusiano wa China na Afrika.”

Mwanafunzi wa semina hiyo Tendai Chirau, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya ZANU-PF ya Zimbabwe alisema, majibu hayo ya barua yaliwatia moyo wanafunzi wote. “Yana maana muhimu kwetu makada vijana wa vyama sita vya Kusini mwa Afrika kujumuika kwenye semina hiyo. Na ni muhimu zaidi kuwa, kwenye semina hiyo tunaweza kujifunza na kufahamishwa kwa kina njia ya maendeleo ya China na uzoefu wa China wa kuondoa umaskini kwenye semina.”

Shule ya Uongozi ya Nyerere ilianzishwa na Chama cha Mapinduzi cha Tanzania (CCM), Chama cha African National Congress cha Afrika Kusini (ANC), Chama cha Ukombozi cha Msumbiji (FRELIMO), Chama cha Harakati ya Ukombozi wa Watu cha Angola (MPLA), Chama cha SWAPO cha Namibia pamoja na Chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe. Ilikamilika na kuanza kutumika Tarehe 23, Februari, mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha