Reli ya Hotan-Ruoqiang yazinduliwa ambayo ni njia ya kwanza ya reli duniani ya kuzunguka jangwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2022
Reli ya Hotan-Ruoqiang yazinduliwa ambayo ni njia ya kwanza ya reli duniani ya kuzunguka jangwa

Juni 16, treni ya 5818 iliyojaa abiria iliondoka kutoka Kituo cha Reli cha Hotan cha Xinjiang, ambapo Reli ya Hotan-Ruoqiang ilianza kufanya kazi. Reli ya Hotan-Ruoqiang, Reli ya Kusini mwa Xinjiang na Reli ya Geku zinaunda njia ya reli yenye urefu wa kilomita 2,712 inayozunguka Jangwa la Taklimakan. Tangu wakati huo, njia ya kwanza ya reli duniani ya kuzunguka jangwa imekamilika ujenzi wake nchini China.

Reli ya Hotan-Ruoqiang ni mradi muhimu wa taifa wa ujenzi wa reli, ambayo iko kwenye ukingo wa kusini mwa Jangwa la Taklimakan, kutoka Mji wa Hotan,kusini-magharibi mwa Xinjiang hadi Wilaya ya Ruoqiang, kusini-mashariki mwa Xinjiang, urefu wake wa jumla ni kilomita 825, na kasi iliyopangwa ni kilomita 120 kwa saa. (Mpiga picha:Dinglei/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha