Kuwafuatilia watoto wa Afrika, kueneza matumaini kwa upendo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 20, 2022
Kuwafuatilia watoto wa Afrika, kueneza matumaini kwa upendo
Maofisa na askari wa Kikosi cha askari wa miguu wa kulinda amani cha China wakitoa zawadi za vitu vya masomo kwa Shule ya Msingi ya Green Sud.

Hivi karibuni wakati siku ya kimataifa ya watoto wa Afrika ilipowadia, Kikosi cha nane cha askari wa miguu wa kulinda amani cha China katika Sudan Kusini (Juba) kilikwenda Shule ya Msingi ya Green Sud iliyoko karibu na UN House kufanya shughuli ya mawasiliano kati ya wanajeshi na watu na kuwaletea vitu vya msaada wa kibinadamu.

Juni 13, 1991, Mfuko wa watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ilitangaza kuwa Juni 16 itakuwa Siku ya Kimataifa ya Watoto wa Afrika ambayo inalenga kutoa wito wa kuwataka watu kufuatilia watoto wa Afrika wanaokumbwa na balaa ya njaa, vita, umaskini na maradhi.

Shule ya Msingi ya Green Sud ina walimu na wanafunzi zaidi ya 480. Katika shule hiyo, majengo na vifaa vya mafunzo ni vya hali duni, ambapo hakuna deski au ubao, madarasa machache tu iliyonayo pia ni ya kikukuu, watoto wakikaa kwenye ardhi wakati wa kusoma. Vitabu vya kusomea, kalamu na karatasi, na mikoba ya shule ni haba zaidi.

Ili kupunguza shinikizo la mafunzo la shule hiyo, kikosi hicho cha China kiliwazawadia watoto vitu vya masomo, vifaa vya burudani na kuwatia moyo wawe na nia thabiti, kusoma kwa bidii ili kupata ujuzi na kutoa mchango kwa ajili ya amani na maendeleo ya Sudan Kusini baada ya kuwa watu wazima.

Baadaye, askari wa kulinda amani walifanya maonesho ya michezo ya Sanaa ya jadi ya China kama vile kubadilisha uso, Wushu, na kucheza dansi kwa kuwafurahisha watoto. Tabasamu tamu zilionekana kwenye nyuso za watoto, na upendo wa askari wa kulinda amani wa China ulifanya shule hiyo kujaa furaha.

Kiongozi wa kikosi hicho Guo Lei alisema kuwa ingawa watoto hawa hawana mazingira mazuri ya maisha na masomo, lakini tabasamu za furaha kubwa kwenye nyuso zao zilituvutia. Watoto ni kama jua la asubuhi, pia ni mustakabali wa nchi, tunawatakia ukuaji mzuri na furaha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha