Kituo kikubwa zaidi cha Asia cha Treni za abiria chaanza kazi Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2022
Kituo kikubwa zaidi cha Asia cha Treni za abiria chaanza kazi Beijing
Picha iliyopigwa Juni 20, 2022 ikionesha kituo cha treni cha Fengtai hapa Beijing, Mji Mkuu wa China. (Picha/Xinhua)

Kituo kikubwa zaidi cha Asia cha treni za abiria kilianza kufanya kazi Jumatatu wiki hii hapa Beijing. Kufanyiwa ukarabati kwa miaka minne kumeleta uhai mpya kwa kituo hicho kikongwe zaidi cha treni cha Beijing, Mji Mkuu wa China.

Eneo la jumla la majengo ya kituo hicho cha treni, yaani kituo cha treni cha Fengtai cha Beijing ni karibu mita za mraba 400,000, ambalo ni sawa na maeneo ya viwanja 56 sanifu vya soka. Kituo hicho kina njia 32 za reli na majukwaa 32, kikiwa na uwezo wa kuwapokea abiria 14,000 kila saa.

Kituo hicho cha treni chenye historia ndefu kiko kwenye eneo la Fengtai la Kusini mwa Beijing. Kilijengwa kuanzia mwaka 1895 na kutoa huduma za kusafirisha abiria na mizigo mpaka kufungwa mwaka 2010. Kazi ya kukikarabati ilianzia mwaka 2018.

Licha ya upanuaji wa majengo ya kufanya kazi, muonekano wa kituo pia umesasishwa kabisa, na unatumia usanifu wa aina mbalimbali za majengo ya jadi ya kichina.

Kituo hicho pia ni kituo cha kwanza chenye muundo wa ghorofa mbili ambacho kinatoa huduma ya treni za mwendo kasi pamoja na treni za kawaida. Chini ya kituo hicho kiko kituo cha sabwe, ambacho kinaleta urahisi kwa watu kubadilisha njia ya usafiri.

Waendeshaji wa kituo hicho walisema, treni 120 zitatumika katika kipindi cha mwanzo cha uendeshaji. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha