Pilikapilika za Bandari ya Qingdao: meli za nchi za BRICS zatia nanga huko kila baada ya dakika mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 22, 2022
Pilikapilika za Bandari ya Qingdao: meli za nchi za BRICS zatia nanga huko kila baada ya dakika mbili
Meli za makontena zikipakia na kupakua makontena kwenye gati la Qianwan la Bandari ya Qingdao ya Shandong, China. (Picha ilipigwa Tarehe 15, Juni/Xinhua)

Kwenye bandari yenye pilikapilika ya Qingdao ya Mkoa wa Shandong, meli za makontena za nchi za BRICS zinapakia na kupakua mizigo huko karibu kila siku. Kwa wastani kila baada ya dakika mbili, kuna shehena moja ya mizigo ya nchi za BRICS kwenye bandari hiyo ambayo inapakuliwa au kupakiwa na kusafirishwa kwa nchi za nje. Takwimu kutoka mamlaka ya forodha ya Qingdao zinaonesha, kutoka Januari hadi Mei mwaka huu, meli zinazotoka Qingdao na kwenda nchi za BRICS moja kwa moja zimesafirisha makontena 830,000, kiasi hicho kimeongezeka kwa asilimia 12 kikilinganishwa na wakati huo wa mwaka jana, na kiasi cha uuzaji wa nje kimeongezeka kwa asilimia 26.1.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha