Tetemeko la ardhi lililotokea Afghanistan lasababisha vifo vya watu zaidi ya 1000

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2022
Tetemeko la ardhi lililotokea Afghanistan lasababisha vifo vya watu zaidi ya 1000
Picha iliyopigwa Juni 22, 2022 ikionesha nyumba iliyoharibiwa katika tetemeko la ardhi kwenye Mkoa wa Paktika, Afghanistan. (Picha/Xinhua)

Ofisa wa ngazi ya mkoa wa Afghanistan alisema, tetemeko la ardhi lililotokea Mashariki mwa Afghanistan mapema Jumatano limesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 na wengine zaidi ya 1,500 kujeruhiwa, akiongeza kuwa idadi ya vifo vya watu na wengine waliojeruhiwa huenda itaendelea kuongezeka.

Mkuu wa Idara ya Upashanaji wa Habari na Utamaduni ya mkoa Mohammad Amin Haddifa aliliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, “zaidi ya watu 1,000 wamefariki na wengine 1,500 wamejeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi na maporomoko ya ardhi inayofuata kwenye eneo la Gayan na Barmal.”

Ofisa wa Mkoa wa Khost alisema, katika mkoa wa Khost ulioko karibu na eneo la tetemeko, nyumba, misikiti na maduka zaidi ya 600 yameharibika, na watu zaidi ya 25 wamefariki na wengine 100 wamejeruhiwa.

Akaunti ya tweet ya ofisi ya Waziri Mkuu ilisema, masaa kadhaa baada ya tetemko la ardhi kutokea, kaimu waziri mkuu Mullah Mohammad Hassan Akhund aliongoza mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri. Pia aliagiza kutenga fedha za afghanis bilioni 1 (zaidi ya Dola za Marekani 1120) ili kuwasaidia watu walioathiriwa na maafa.

Tetemeko hilo la ardhi lilitokea kilomita 44 Kusini Magharibi kutoka Khost likiwa na ukubwa wa 5.9 kwenye vipimo vya Ritcher.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha