Xi Jinping: Nchi za BRICS zinapaswa kuwajibika na kuleta nguvu ya hamasa, utulivu na ya kiujenzi kwa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2022
Xi Jinping: Nchi za BRICS zinapaswa kuwajibika na kuleta nguvu ya hamasa, utulivu na ya kiujenzi kwa Dunia
Rais Xi Jinping wa China akiwa mwenyeji wa Mkutano wa 14 wa Wakuu wa nchi za BRICS kupitia njia ya video mjini Beijing, China. (Picha/Xinhua)

BEIJING: Jioni ya Juni 23, Rais Xi Jinping wa China alikuwa mwenyeji wa Mkutano wa 14 wa Wakuu wa nchi za BRICS mjini Beijing, China kupitia njia ya video.

Rais Xi amedhihirisha kuwa katika mwaka mmoja uliopita, Dunia imekabiliana na hali ya kuendelea kuenea kwa UVIKO-19, taabu za ufufukaji wa uchumi wa Dunia na matatizo mazito zaidi ya amani na usalama. Kwa kukabiliwa na changamoto na hali yenye utatanishi, nchi za BRICS zikifuata moyo wa BRICS wa kufungua milango, shirikishi na ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha mshikamano na kufanya juhudi za kukabiliana na changamoto kwa pamoja. Amsema, mfumo wa BRICS umeonyesha uthabiti na uhai. Ushirikiano wa BRICS umepata maendeleo na matokeo mazuri.

Rais Xi amesisitiza kuwa Mkutano huu unafanyika katika wakati muhimu wa kuunda mwelekeo wa siku zijazo za binadamu. Nchi za BRICS, zenye soko muhimu linaloibuka na nchi kubwa zinazoendelea, zinahitaji kubeba wajibu na kuleta nguvu ya hamasa, utulivu na ya kiujenzi kwa Dunia.

Rais Xi amesema: Kwanza, tunatakiwa kutoa sauti kwa ajili ya usawa na haki. Tunahitaji kuhimiza jumuiya ya kimataifa kutekeleza mfumo wa pande nyingi kwa ukweli na kushikilia mfumo wa kimataifa ambao Umoja wa Mataifa ukiwa msingi wake, na kutekeleza utaratibu wa kimataifa unaosimamiwa na sheria za kimataifa, na kutoa wito kwa Dunia kukataa mawazo ya Vita Baridi na makabiliano ya kambi, kupinga vikwazo vya upande mmoja na matumizi mabaya ya vikwazo, na kukataa miduara midogo inayojengwa kutumikia siasa za umwamba, na kuunda familia moja kubwa kwenye jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Pili, tunatakiwa kushikilia ushirikiano na maendeleo, na kukabiliana kwa pamoja na hatari na changamoto. Kushikilia nia yetu ya kushinda janga la virusi vya Korona na kuchukua hatua kwa uwajibikaji kulinda watu wetu na maisha yao. Tunahitaji kujenga njia thabiti ya kujilinda dhidi ya virusi, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa kukabiliana na UVIKO, na kutetea kwa pamoja maisha na afya ya watu.

Tatu, tunahitaji kuunganisha nguvu kwa ajili ya ufufukaji wa uchumi, kuongeza uratibu wa sera za uchumi mkuu, kuweka minyororo ya viwanda na ugavi katika usalama na bila kufungwa, kujenga uchumi wa Dunia ulio wazi, na kuzuia na kupunguza hatari na changamoto kubwa katika maendeleo ya kimataifa, kufanya kazi kwa ajili ya uchumi shirikishi na imara zaidi.

Nne, tunapaswa kutetea maendeleo endelevu na yanayozingatia watu, kuwekeza zaidi katika kupunguza umaskini, chakula, elimu, afya na kadhalika, na kuendeleza utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ya 2030, ili kuleta maendeleo mazuri yenye nguvu, na bila kuchafua mazingira duniani.

Rais Xi amesema anatarajia mjadala wa kina na mahiri chini ya mada ya "Kuhimiza Ushirikiano wenzi wa kiwango cha juu na kuanzisha zama mpya ya maendeleo ya dunia " ili kuchangia kwa pamoja hekima na mawazo katika maendeleo ya kiwango cha juu ya ushirikiano wa BRICS. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha