Migomo ya wafanyakazi yalazimisha shirika la umeme la Afrika Kusini kuchukua hatua kali za kukata umeme

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2022
Migomo ya wafanyakazi yalazimisha shirika la umeme la Afrika Kusini kuchukua hatua kali za kukata umeme
Watu wakisubiri kuvuka barabara wakati wa kukatwa kwa umeme huko Cape Town, Afrika Kusini, Juni 28, 2022. Shirika la Umeme la Afrika Kusini, Eskom Jumanne wiki hii limetangaza kwamba lilibadilisha kiwango cha uzalishaji umeme kutoka Hatua ya 4 ya sasa hadi hatua kali zaidi ya 6 katika baadhi ya vipindi siku za Jumanne na Jumatano, ikitoa sababu ya mgomo wa wafanyakazi unaohusiana na madai ya mishahara ambao umesababisha kutatiza mitambo ya shirika hilo. (Xinhua/Lyu Tianran)

CAPE TOWN - Shirika la Umeme la Afrika Kusini, Eskom Jumanne wiki hii limetangaza kwamba limebadilisha kiwango cha uzalishaji umeme kutoka Hatua ya 4 ya sasa hadi hatua kali zaidi ya 6 katika baadhi ya vipindi siku za Jumanne na Jumatano, ikitoa sababu ya mgomo wa wafanyakazi unaohusiana na madai ya mishahara ambao umesababisha kutatiza mitambo ya shirika hilo.

Hili ni tatizo baya zaidi la kukatika kwa umeme tangu Mwaka 2019. Eskom imetekeleza hatua ya 6 ya kupunguza kiwango cha uzalishaji wa umeme mara moja tu, Desemba 2019. Shirika hilo limesema katika taarifa yake kuwa hatua ya 6 ya upunguzaji wa umeme ilitekelezwa kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni kwa siku ya Jumanne na saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni kwa leo Jumatano, wakati Hatua ya 4 au Hatua ya 2 itatekelezwa wakati wa saa nyingine.

Eskom imesema hatua hiyo ya wafanyakazi imesababisha usumbufu mkubwa kwenye mitambo yake ya kuzalisha umeme, ambayo inalazimu kuendelea kuchukua hatua za tahadhari ili kuhifadhi uwezo wa uzalishaji na kulinda mitambo dhidi ya uharibifu.

Kabla ya tangazo hilo, Ijumaa ya wiki iliyopita Eskom ilisema itahamisha kiwango cha kuzalisha umeme kutoka Hatua ya 2 hadi Hatua ya 4 mara nyingi kuanzia Ijumaa hadi Jumapili kutokana na "mgomo wa wafanyakazi usiyodhibitiwa", kufuatia mkwamo wa mazungumzo ya mishahara.

Siku ya Jumapili, Eskom iliamua kuongeza Hatua ya 4 hadi Jumatano hii baada ya mgomo wa wafanyakazi katika vituo vya umeme kuathiri matengenezo na ukarabati uliopangwa.

Eskom imesema kwa sasa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 3,218 (MW) iko kwenye matengenezo yaliyopangwa, wakati mitambo mingine yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawati 17,621 haifanyi kazi kwa sababu ya kuharibika.

Vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikidai nyongeza ya mishahara ya asilimia 10 huku Eskom ikitoa nyongeza ya asilimia 5.3 tu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha