Barabara mpya ya mwendo kasi yafunguliwa kwenye Jangwa kubwa zaidi la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2022
Barabara mpya ya mwendo kasi yafunguliwa kwenye Jangwa kubwa zaidi la China
Picha iliyopigwa kutoka angani ikionesha barabara mpya ya mwendo kasi ikipita Jangwa la Taklimakan katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, Kaskazini Magharibi mwa China, Juni 23, 2022. (Xinhua/Li Xiang)

Barabara mpya ya mwendo kasi inayopita Jangwa la Taklimakan katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur wa Kaskazini Magharibi mwa China lilifunguliwa Alhamisi wiki hii

Barabara hiyo ya mwendo kasi ipo kwenye Eneo linalojiendesha la kabila la wamongolia la Bayingolin, Kusini mwa Mkoa wa Xinjiang, na inaunganisha Wilaya ya Yuli na Wilaya ya Qiemo ikiwa ni barabara ya tatu ya mwendo kasi inayopita Jangwa la Taklimakan, jangwa la mchanga unaohamahama ambalo ukubwa wake ni wa pili duniani.

Kasi ya barabara hiyo inayopangwa ni kilomita 60 au 80 kwa kila saa kutokana na kipindi, na urefu wake kwa jumla ni kilomita 334, na sehemu ya kilomita 307 ya barabara hiyo inapita eneo la jangwa. Hadi hivi sasa, kuna barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 1200 inayopita Jangwa la Taklimakan nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha