

Lugha Nyingine
Tukio la kufyatua risasi kwenye Kituo cha ununuzi bidhaa cha Mji Mkuu wa Denmark lasababisha vifo vya watu wengi
Tarehe 3 polisi wa Denmark walithibitisha kuwa, tukio la kufyatua risasi lilitokea kwenye kituo cha ununuzi bidhaa cha Kusini mwa Copenhagen, Mji Mkuu wa Denmark saa 9 mchana kwa saa za huko, likasababisha vifo vya watu wengi. Askari polisi walikamata mwanamume mwenye umri wa miaka 22 wa Denmark karibu na kituo hicho cha ununuzi bidhaa.
Mkuu wa ofisi ya idara ya polisi ya Copenhagen Soren Thomassen kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye sehemu ya tukio hilo alisema, tukio hilo limesababisha vifo vya zaidi ya mtu mmoja, pamoja na wengine wengi kujeruhiwa. Lakini hajataja idadi ya watu waliofariki na kujeruhiwa.
Bw. Thomassen pia alisema, hivi sasa bado hawajaweza kuondoa uwezekano wa kuwa tukio hili ni la ugaidi. Askari polisi wamefunga eneo karibu na kituo hicho, na kuanza kufanya operesheni kubwa katika kisiwa kizima cha Zealand, pamoja na mji wa Copenhagen.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma