Magari ya China yanayoweza kuendeshwa mbugani yaonekana kwa mara ya kwanza nchini Saudi Arabia (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2022
Magari ya China yanayoweza kuendeshwa mbugani yaonekana kwa mara ya kwanza nchini Saudi Arabia
Gari la "Tank 300" linaloweza kuendeshwa mbugani likionyeshwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Riyadh, Saudi Arabia, Tarehe 3 Julai 2022. (Xinhua/Wang Haizhou)

RIYADH – Magari mawili yanayoweza kuendeshwa mbugani yanayoundwa na Kampuni ya Great Wall Motor ya China yameonekana kwa mara ya kwanza nje ya China katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

"Tank 300" na "Tank 500" ni mifano miwili ya magari kutoka kwa chapa ya "Tank" ya kampuni hiyo, inayolenga kuingia kwenye soko la kimataifa.

"Mashariki ya Kati ndilo soko kuu lenye uwezekano mkubwa la magari ya kuendeshwa mbugani katika dunia , na pia ni soko linalopendekezwa kwa utandawazi wa chapa ya 'Tank'," amesema Xu Huanzhi, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Great Wall Motor, Kanda ya Mashariki ya Kati kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumapili usiku.

Gautam Arun, Mkurugenzi wa Bidhaa wa Kampuni ya Great Wall Motor, Kanda ya Mashariki ya Kati, amesema modeli ya "Tank 300" inatoa tajiriba mpya ya kuendesha mbugani inayohudumia ubinafsi wa watumiaji, na inavunja vizuizi kati ya SUV zinazoendeshwa mbugani na SUV zinazoendeshwa mijini kwenye barabara.

Takwimu za masoko zilizotolewa na Great Wall Motor zinaonyesha kuwa kiwango cha ukuaji wa kampuni hiyo katika soko la Saudi Arabia kutoka Mwaka 2018 hadi 2021 kilifikia asilimia 204, na kiasi cha mauzo yake ni cha juu miongoni mwa chapa za China za magari nchini Saudi Arabia.

"Magari ya China, hasa ya kifahari, yanazidi kuwa maarufu miongoni mwa wanunuzi wa Saudi Arabia kwa sababu ya ubora na huduma zao," amesema Majed Yahya, Mkurugenzi Mkuu wa ADMC, wakala mkuu wa Great Wall Motor nchini Saudi Arabia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha