Maoni: Utawala unaodumaa, mfumo wa kifisadi ni sababu ya shambulio la risasi Siku ya Uhuru wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2022
Maoni: Utawala unaodumaa, mfumo wa kifisadi ni sababu ya shambulio la risasi Siku ya Uhuru wa Marekani
Watu wakipeperusha bendera za Taifa za Marekani kwenye National Mall kusherehekea Siku ya Uhuru ya Marekani mjini Washington, D.C., Marekani, Julai 4, 2022. (Picha na Aaron Schwartz/Xinhua)

BEIJING – Mashambulizi mawili ya risasi katika siku moja, na Julai 4. Wikiendi ya sherehe za Siku ya Uhuru wa Marekani za mwaka huu, wakati Wamarekani wakisherehekea utaifa kwa kanivali na gwaride, walikumbwa na vurugu za kutisha za ufyatuaji risasi.

Takriban watu sita wameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi katika gwaride la Julai 4 lililofanyika katikati ya Kitongoji cha Highland Park, Illinois, huku wengine kwa makumi wakijeruhiwa. Saa chache baadaye, maafisa wawili wa polisi waliripotiwa kupigwa risasi huko Philadelphia, mji mkubwa zaidi wa Pennsylvania, wakati wa maonyesho ya fataki ya Siku ya Uhuru.

"Katika siku ambayo tulikusanyika kusherehekea jamii na uhuru, badala yake tunaomboleza kupoteza maisha," alisema Meya wa Highland Park, Nancy Rotering.

Kwa Wamarekani, hakuna mahali pa uzalendo zaidi kusherehekea Siku ya Uhuru kuliko Philadelphia. Lakini mahali hapo ambapo Uhuru wa Marekani ulizaliwa sasa kumetiwa doa na vurugu na kugubikwa na mshtuko, huzuni na hasira.

Mashambulizi hayo ya risasi yanaongeza ukurasa mwingine wa kuumiza moyo kwa rekodi ya kutisha ya Marekani na inayoonekana kutoweza kudhibitiwa ya vurugu za kutumia bunduki.

Kwa mujibu wa asasi ya utafiti isiyo ya faida ya Kumbukumbu za Vurugu za Bunduki, angalau visa 310 vya kufyatua risasi vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 22,000 hadi kufikia sasa mwaka huu.

Umwagaji damu katika Siku ya Uhuru kwa mara nyingine tena umeweka wazi vurugu za bunduki kama uvimbe unaoitesa jamii ya Marekani, ukigawanya taifa hilo mara kwa mara na kuondoa imani ya umma katika uwezo wa kutawala wa Serikali ya Marekani.

Jambo baya zaidi, Mahakama ya Juu ya Marekani, ambayo ni mamlaka ya juu zaidi ya kutetea Katiba ya nchi hiyo, iliongeza mvutano juu ya udhibiti wa bunduki mwishoni mwa mwezi wa Juni kwa kufuta sheria ya zamani ya Jimbo la New York inayowataka wamiliki wa bunduki kuwa na sababu halali ili kubeba silaha kwa siri.

Haki ya kuishi ni haki ya asili na isiyoweza kuondolewa, lakini inaonekana kwamba baadhi ya viongozi Washington hawafikiri hivyo. Huku wakiimba "uhuru dhidi ya woga" kuwa haki ya kuzaliwa ya kwanza kwa kila mtu, wamefanya juhudi ndogo kupunguza mgawanyiko wa kisiasa na kuhakikisha usalama wa Wamarekani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha