Chuo cha ufundi wa kazi chasaidia vijana wa Rwanda kupata ajira (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 13, 2022
Chuo cha ufundi wa kazi chasaidia vijana wa Rwanda kupata ajira
Tarehe 8, Julai, 2022, mwanafunzi akifanya mazoezi ya kudhibiti mashine mazito kwenye chuo cha ufundi wa kazi Forever cha Kigali, Rwanda. (Picha/Xinhua)

Chuo cha ufundi wa kazi Forever kilichoko Kigali, mji mkuu wa Rwanda kinatoa mafunzo ya ufundi wa kazi ili kuwawezesha wanafunzi vijana wapate nafasi zaidi katika soko la ajira.

Chuo hicho kilianzishwa na kampuni ya teknolojia ya China Beijing Forever mnamo mwaka 2018, kikitoa mafunzo ya kazi kuhusu udhibiti wa mashine mazito, umeme wa viwanda, ujenzi wa barabara, uhandisi wa kompyuta n.k.

Mkuu wa chuo hicho Narcisse Iziabayo alisema, chuo hicho ni moja ya vyuo bora vya ufundi wa kazi. “Tunatoa mafunzo yasiyopatikana katika sehemu nyingine za ukanda huo, kuhusu kazi za utunzi na udhitibi wa mashine mazito,” alisema.

Aliongeza kuwa, mshahara wa kila mwezi wa wahitimu wa chuo hicho ni kutoka faranga ya Rwanda laki 1 hadi 5 (kutoka dola za Marekani 97 hadi 487), na wanaajiriwa na kampuni kubwa za Rwanda na kampuni za China.

Chuo hicho sasa kina wanafunzi 154. Tangu kilipoanzishwa mwaka 2018, kimewaandaa wahitimu karibu 500 wa ufundi wa kazi mbalimbali.

Kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi Jerome Uwimpuhwe alisema anafurahia kuwa mwendeshaji wa mashine mazito. “Tukiwa vijana tumepata mafunzo yanayotusaidia kukabiliana na changamoto za maisha yetu,” alisema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha