

Lugha Nyingine
Makala: Mwanamke Mjasiriamali kutoka China anayeboresha maisha ya watu nchini Rwanda
KIGALI - Mwanamke Mjasiriamali wa China Yang Jing anaweza kuwa asiwe mtu wa kwanza kukumbuka anapofikiria uhisani, lakini hilo ndilo hasa ambalo amelenga kufanya katika muongo mmoja uliopita.
Tangu alipoanza kufanya shughuli zake, Yang Jing, mmiliki wa Hoteli ya Dmall huko Kigali, Mji Mkuu wa Rwanda, anasema amesaidia mamia ya watoto nchini China na kote barani Afrika akilenga watu binafsi na makundi.
Mwezi Mei, katika mchango wake wa hivi majuzi zaidi alienda kwenye shule ya msingi na sekondari ya Tanda (GS Tanda), shule yenye wanafunzi takriban 1,500 Kaskazini mwa Rwanda. Ikishirikiana na Jumuiya ya Wachina wa Ng'ambo, Hoteli ya Dmall ilitoa yuan 500,000 (kama dola 74,557 za Kimarekani) kwa shule hiyo, ikiwa ni pamoja na vifaa vya elimu, chakula, vyombo vya kulia chakula, mipira, na viatu.
"Nimekuwa nikijitolea kwenye uhisani kwa takriban miaka 10 iliyopita. Mawazo yangu daima ni kufanya juhudi niwezavyo kusaidia wale wanaohitaji na kutoa matumaini na ukarimu," Yang ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano.
Providence Uwiringiyimana, mwanamke wa Rwanda mwenye umri wa miaka 27, ni mmoja wa watu ambao wamefaidika na moyo wa ukarimu wa Yang. Alipohitimu kutoka shule ya sekondari Mwaka 2016, kuendelea hadi chuo kikuu kulionekana kama matarajio yenye wasiwasi, lakini hii haikukatisha ndoto ya Uwiringiyimana kitaaluma.
Miaka mitatu baadaye, kwa sababu ya msaada wa Yang, Uwiringiyimana sasa ni mhitimu wa usimamizi wa hoteli na mikahawa kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Utalii na Mafunzo ya Biashara (UTB) nchini Rwanda, akiwa mwenye furaha na ana uhakika zaidi kuhusu siku zijazo.
"Kusoma Chuo kikuu ni gharama kubwa lakini watu wema kama Yang wanaosaidia watu ambao hawawezi kumudu elimu, wana thamani kubwa," ameliambia Xinhua. "Mahitaji yoyote ya kitaaluma niliyohitaji ikiwa ni pamoja na ada, Yang alikuwa tayari kunisaidia kando na kulipa mshahara. Kama mfanyabiashara, nimejifunza mengi kutoka kwake. Ananichukulia kama dada yangu mkubwa."
Yang anamtaja Uwiringiyimana kama mwanamke mwerevu na mchapakazi wa Rwanda ambaye alianza kumfanyia kazi za ndani akiwa na umri wa miaka 23.
"Nia yake ya kwenda chuo kikuu ilijidhihirisha kwa nguvu, lakini hitaji lake la kazi lilikuwa kubwa pia," Yang amesema.
Shirika lingine la nchini Rwanda ambalo limefaidika na uhisani wa Yang ni Empower, Develop Dignify (EDD) katika Wilaya ya Gasabo ya Kigali, ambalo linalenga kusaidia watoto wapatao 120 waliochukuliwa kutoka mitaani ili wasome katika shule mbalimbali nchini humo.
“Mwanzoni Yang alitoa vifaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nguo kwa shirika hilo,” anasema Charles Hazabintwali, Mkurugenzi Mtendaji wa EDD.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma