Bustani ya Wanyama ya Chongqing yawasaidia wanyama kuepuka joto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2022
Bustani ya Wanyama ya Chongqing yawasaidia wanyama kuepuka joto
Mfugaji akiwaogesha panda ili kuwasaidia kuepuka joto. (Mpiga picha: Zou Le)

Siku za hivi karibuni, Chongqing inaendelea kuwa na hali ya joto kali. Ili kuwasaidia wanyama kuepuka joto, Bustani ya Wanyama ya Chongqing imeandaa vifaa mbalimbali vya kuepusha joto wakati wa majira ya joto kwa ajili ya wanyama.

Mkuu wa ofisi ya usimamizi wa wanyama wa Bustani hiyo Tang Jiagui alijulisha kuwa baada ya kuingia majira ya joto, Bustani ya Wanyama ya Chongqing siyo tu inaongeza vyakula vya kusaidia kuepusha joto kwa ajili ya wanyama, kama vile tikitimaji na matango, pia inatengeneza matunda ya barafu kwa kuwalisha wanayma. Zaidi ya hayo, bustani hiyo inaongeza vifaa vipya ili kuepusha joto kwenye mazingira ya wanyama waliko.

Wakati wa joto kali katika majira ya joto, bustani inaweza kuwawezesha wanyama wapate mapumziko zaidi. Tang Jiagui alipendekeza kuwa wakati wa majira ya joto, ni bora watembeleaji wachague asubuhi kwenda bustani.

Zaidi ya hayo, wafanyakazi walinunua mapema dawa za kuepuka joto na kuzitia kwenya chakula au maji ya wanyama ili kuzuia wanyama kupatwa na ugonjwa wa joto. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha