Mabadiliko makubwa kwenye njia za vijijini katika Mlima Daliangshan (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2022
Mabadiliko makubwa kwenye njia za vijijini katika Mlima Daliangshan

Hali ya kijioglafia ya Tarafa inayojiendesha ya Wayi ya Liangshan ya Mkoa wa Sichuan ni yenye utatanishi wa kihatari, vizuizi vya kijiografia vilivyotokana na milima mirefu na mabonde vilikuwa matatizo kwa kazi ya kuboresha usafiri kwenye eneo hili. Katika miaka ya hivi karibuni, tangu uanze kutekelezwa kwa mkakati wa kuondoa umaskini hadi kustawisha vijiji, mabadiliko makubwa yametokea katika hali ya usafiri kwenye eneo la Mlima Liangshan.

Takwimu zinaonesha kuwa hadi Mwezi Juni, Mwaka 2022, wilaya na vijiji vyote vinavyofaa kwenye eneo la Mlima Liangshan vimefikika kwa mabasi ya abiria. Hadi mwisho wa Mwaka 2021, jumla ya urefu wa barabara za vijijini katika Tarafa ya Mlima Liangshan umefikia kilomita 24,500.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha