Maua adimu ya Yungiyungi yachanua Puzhehei mkoani Yunnan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2022
Maua adimu ya Yungiyungi yachanua Puzhehei mkoani Yunnan
Maua adimu ya Yungiyungi ya aina ya “Dasajin” yakichanua katika majira ya joto. (Picha kutoka Kituo cha Media Jumuishi cha Wilaya ya Qiubei)

Mwezi Julai, Maua adimu ya Yungiyungi ya aina ya “Dasajin” yamechanua katika eneo la vivutio vya taifa la Puzhehei la ngazi ya AAAAA,ambayo nusu ya petali zao ni rangi nyekundu, na nyingine ni rangi nyeupe.

Maua ya“Dasajin”ni aina moja ya maua adimu ya Yungiyungi pori yanayokua huko Puzhehei. Kutokana na utafiti na uthibitisho wa wataalamu wa Taasisi ya Utafiti wa Maua ya Yungiyungi ya China, aina mbili ya maua ya Yungiyungi yaani “Dasajin” na “Xiaosajin” zinazokua huko Puzhehei ziko hatarini kutoweka katika sehemu nyingine duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha