"Kushindwa kwa mfumo" kwatajwa kusababisha shambulio la risasi lililoua watu 21 katika shule ya Uvalde huko Texas, Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2022
Watu wakiomboleza kwa ajili ya waathirika wa shambulio la risasi kwenye halaiki shuleni katika eneo la Town Square huko Uvalde, Texas, Marekani, Mei 30, 2022. (Xinhua/Wu Xiaoling)

HOUSTON - Ripoti ya kamati ya uchunguzi ya Bunge la Texas, Marekani iliyotolewa Jumapili imeonesha kuwa "kushindwa kwa mfumo" kumesabisha shambulio la Mei 24 la shule ya msingi na kuua watoto 19 na walimu wawili huko Uvalde, Jimbo la Texas, Kusini mwa Marekani.

Ripoti hiyo yenye kurasa 77 ambayo ni kamilifu zaidi ya kuwajibika kwa matukio ya ufyatuaji risasi hadi sasa, inaeleza kuwa takriban maafisa 376 wa kusimamia utekelezaji wa sheria walikimbilia katika Shule ya Msingi ya Robb muda mfupi baada ya mpiga risasi mmoja, Salvador Ramos kufyatua risasi -- wengi wao wakiwa wasimamizi wa utekelezaji sheria wa serikali kuu na wa jimbo wenye majukumu ikiwa ni pamoja na kujibu dhidi ya mashambulizi katika maeneo ya umma.

“Hata hivyo, hakuna hata mmoja wao aliyeweza kumshinda kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 kabla ya kutekeleza tukio la hilo kufyatua risasi ambalo ni la pili kiathari katika historia ya Marekani, kwa sababu ya "kushindwa kwa mfumo na kufanya maamuzi mabaya," inasema ripoti hiyo.

Polisi wa eneo hilo, hasa Pete Arredondo, ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa polisi wa Wilaya ya Uvalde Consolidated Independent School District (CISD), walikosolewa kwa kiasi kikubwa kwa kushindwa kufuata mafundisho tendaji yaliyoanzishwa baada ya mauaji ya Mwaka 1999 katika Shule ya Sekondari ya Columbine, ambayo yanaamuru kwamba maafisa wakabiliane na washambuliaji mara moja. Badala yake, Arredondo hakuchukua jukumu, na polisi wa eneo hilo walirudi nyuma baada ya kufyatuliwa risasi na kusubiri usaidizi.

"Walishindwa kuweka kipaumbele kuokoa maisha ya waathiriwa wasio na hatia badala ya usalama wao," ripoti hiyo imesisitiza ukosoaji huo.

Na "maafisa hawa wa eneo hilo siyo tu waliotarajiwa kusambaza uongozi unaohitajika wakati wa mkasa huu," ripoti imebainisha. "Katika shambulio hili, hakuna polisi aliyechukua hatua ya kuchukua nafasi ya kutoa amri kwenye tukio hilo."

"Licha ya hali ya wazi ya machafuko, maafisa wa polisi wenye vyeo wa idara zingine za usalama za kukabiliana na mashambulizi hawakwenda kwa mkuu wa polisi wa Uvalde CISD au mtu mwingine yeyote aliyechukuliwa kuwa mtoa amri kwenye tukio hilo, hali inayoonyesha ukosefu na haja ya nafasi ya kutoa amri, au kutoa msaada maalumu," imesema ripoti.

Ripoti hiyo pia imebaini kuwa utamaduni wa kuridhika ulidhoofisha ulinzi wa Shule ya Msingi ya Robb kwani wafanyakazi mara nyingi waliacha milango wazi.

"Kama wafanyakazi wa shule wangefunga milango kama sera ya shule inavyotaka, hilo lingeweza kupunguza kasi ya mashambulizi” imesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha