China yahamisha wakazi wa Wilaya iliyoko kwenye mwinuko wa juu zaidi kutoka usawa wa bahari ili kuboresha maisha yao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 20, 2022
China yahamisha wakazi wa Wilaya iliyoko kwenye mwinuko wa juu zaidi kutoka usawa wa bahari ili kuboresha maisha yao
Picha iliyopigwa kutoka angani tarehe 27, Machi, 2022 ikionesha mandhari ya Wilaya ya Tsonyi ya Mkoa unaojiendesha wa Tibet wa China.

Wilaya ya Tsonyi ya Mkoa unaojiendesha wa Tibet wa China iko kwenye mwinuko wa juu zaidi kutoka usawa wa bahari duniani. Jumanne ya wiki hii, kundi la pili la wakazi wa wilaya hiyo lilianza kuhama, na hii ni sehemu ya mpango wa eneo hilo la kuboresha maisha ya wakazi na kulinda mazingira ya asili yenye hali dhaifu huko.

Saa 1 na dakika 40 asubuhi ya Jumanne kwa saa za huko, wakazi zaidi ya 300 walikuwa wakiondoka maskani yao kwenye mji mdogo wa Doima wa wilaya hiyo, wakahamia sehemu ya Kusini kwa karibu kilomita 1,000 na kufika maskani yao mapya Singpori.

Singpori iko kwenye kando ya Kaskazini ya Mto Yarlung Zangbo na mwinuko wake ni wa mita 3600 kutoka usawa wa bahari. Ina kilomita 10 tu kutoka uwanja wa ndege wa Lhasa, mji mkuu wa mkoa wa Tibet.

Ifikapo mwanzo mwa Agosti, kazi ya kuhamisha watu wa miji midogo minne ya wilaya hiyo itakamilika, ambapo kazi ya uhamishaji wa wakazi wa miji 7 yote ya Tsonyi, wakiwemo pamoja na wakazi wa miji mitatu waliohamishwa mwaka 2019 itamalizika kabisa.

“Baada ya kuhamia maskani mapya, ninaweza kwenda kwa mahekalu ya Lhasa na Shannan kuabudu Buddha kwa mara nyingi zaidi,” alisema Garma, mfugaji mwenye umri wa miaka 70 kutoka mji wa Doima.

Katika Wilaya ya Tsonyi, wastani wa mwinuko wake ni zaidi ya mita 5,000 kutoka usawa wa bahari, na eneo la mwinuko huo ni la kilomita za mraba 120,000, wilaya hiyo ni sehemu moja ya hifadhi ya mazingira ya asili ya kitaifa ya Changtang, ambayo ni hifadhi kubwa zaidi na iliyoko kwenye mwinuko wa juu zaidi kutoka usawa wa bahari nchini China.

Wilaya hiyo ni sehemu ambayo haifai kuishi kwa binadamu kutokana na mwinuko wake wa juu kutoka usawa wa bahari na mazingira yake yenye hali mbaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha