

Lugha Nyingine
Treni iliyobeba magari ya China yaanza safari ya majaribio kutoka Chongqing hadi Moscow, Russia
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 22, 2022
CHONGQING – Treni ya mizigo ya JSQ ya Shirika la Reli la China maalumu kwa mizigo, ikiwa limepakia magari 207 yaliyoundwa na Kampuni ya Changan Automobile ya China, iliondoka kwenye Stesheni ya Yuzui, katika Mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China siku ya Alhamisi kwa safari yake ya kwanza ya majaribio kuelekea Moscow, Russia.
Muda wa usafirishaji kutoka Chongqing hadi Moscow utapunguzwa hadi siku 18 kwa kutumia huduma ya treni hiyo ya mizigo inayotoa huduma kati ya China na Ulaya, ikilinganishwa na siku 35 kwa kutumia usafiri wa baharini.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma