Kutumia njia za usimamizi wa mazao za majini, ardhini, na angani kuweka msingi kwa mavuno Heilongjiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 22, 2022
Kutumia njia za usimamizi wa mazao za majini, ardhini, na angani kuweka msingi kwa mavuno Heilongjiang
Mitambo ya kuvuna ikifanya kazi katika Shamba la Keshan.

Wakati huu ndio kipindi muhimu cha shughuli za usimamizi wa kazi za mashambani. Ili kuharakisha mchakato wa kukua kwa mimea ya mazao, mashine za kumwaga maji, za kusimamia hali ya ardhini, droni za kunyunyiza dawa, na droni za uhifadhi wa mimea zimetumiwa na kufanya kazi kwenye mashamba mengi ya Jangwa Kubwa la Kaskazini la Mkoa wa Heilongjiang, ambapo zinasimamia hali ya mashamba, kuondoa nyasi na kuwazuia wadudu wanaoleta magonjwa mimea ya mpunga, mahindi na viazi mviringo.

Shughuli za usimamizi wa mashambani katika majira ya joto zinaweka mkazo katika kuongeza joto na kuhifadhi maji kwenye udongo, na mashamba mengi yanaanza shughuli za usimamizi wa mashambani kwa wakati kulingana na hali ya ukuaji wa mimea ya mazao, kuimarisha hatua za kuondoa nyasi na kuzuia wadudu wanaoleta magonjwa mimea, kuhakikisha mazao ya kila aina yanakomaa katika hali ya kawaida, kutimiza usimamizi wa vigezo na kuhakikisha mavuno makubwa ya mazao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha