Baada ya muongo uliopita, eneo la kituo cha mapinduzi cha zamani lafuata njia mpya ya maendeleo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 25, 2022
Baada ya muongo uliopita, eneo la kituo cha mapinduzi cha zamani lafuata njia mpya ya maendeleo
Mwanakijiji akifanya kazi kwenye banda la mboga katika Kijiji cha Tantou cha Ganzhou, Mkoa wa Jiangxi wa Mashariki mwa China Aprili 29, 2021. (Xinhua/Wan Xiang)

Mji wa Ganzhou, Mkoa wa Jiangxi wa Mashariki mwa China uko katika eneo la mlimani la mbali, ulikuwa na nafasi muhimu katika shughuli za mapinduzi ya China zamani kutokana na hali yake ya kijioglafia ambayo ilifaa kwa wakati wa vita. Lakini hali hiyo ya kijiografia imeleta changamoto kwa maendeleo ya hivi sasa.

Mwaka 2012, China ilitoa mkakati wa maendeleo wa kustawisha maeneo ya vituo vya mapinduzi vya zamani, tangu hapo maendeleo ya uchumi na maisha ya watu wa mji wa Ganzhou umeboreshwa sana.

Thamani ya uzalishaji wa viwanda vya fanicha za kisasa vya mji wa Ganzhou ilizidi Yuan bilioni 200 mwaka 2021, huku mapato ya viwanda vya vitambaa na nguo yakizidi Yuan bilioni 100.

Kutoka umaskini hadi ustawi

Ilipofika mwaka 2021, bado kulikuwa na watu maskini karibu milioni 2.2 katika mji wa Ganzhou, kiwango cha umaskini cha mji huu kilikuwa juu zaidi ya wastani wa kile cha nchi nzima ambapo, watu milioni 2.4 hivi wa mji wa Ganzhou hawakuweza kupata maji safi, na familia 71,000 walikosa umeme.

Matumaini yalikuja huko mwaka 2012, ambapo hatua 21 za kitaifa zilitekelezwa mjini Ganzhou, zikiwasaidia wakulima karibu milioni 3 wa Ganzhou kujenga nyumba salama na safi na kujenga barabara za saruji katika vijiji ambavyo kila kijiji ni chenye familia zaidi ya 25.

Kutoka milima hadi dunia

Miundombinu mibovu ilizuia maendeleo ya maeneo ya vituo vya mapinduzi vya zamani, lakini mtandao kamilifu wa mawasiliano wa hivi sasa umeleta fursa nyingi zaidi kwa mji wa Ganzhou.

Ingawa ilikumbwa na janga la maambukizi ya virusi vya korona, Kampuni ya Viwanda ya Jiangxi Rui’en kila wiki husafirisha makontena matatu au matano yanayobeba fanicha kwa Ulaya, Asia Kusini-Mashariki na kanda nyingine.

Mkuu wa kampuni hiyo Luo Liangbing alisema, “kampuni zilizo kwenye maeneo ya vituo vya mapinduzi vya zamani zinaweza kunufaika na gharama za usafirishaji na utaratibu wa kupita forodha na huduma nyingine sawasawa na miji iliyoko kwenye pwani.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha