Waandaaji wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 watangaza kauli mbiu rasmi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2022
Waandaaji wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 watangaza kauli mbiu rasmi
Mkurugenzi wa Chapa wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024 Julie Matikhine akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Paris, Ufaransa, Julai 25, 2022. Huku ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris 2024, waandaaji wa michezo hiyo Jumatatu wiki hii wametangaza "Ouvrons Grand Les Jeux", ikimaanisha "Michezo yenye Uwazi Mpana", kuwa kauli mbiu rasmi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Joto ya Paris. (Xinhua/Gao Jing)

PARIS - Huku ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Paris Mwaka 2024, waandaaji wa michezo hiyo Jumatatu wiki hii wametangaza "Ouvrons Grand Les Jeux"," (Games Wide Open") ikimaanisha "Michezo iliyo Wazi", kuwa kauli mbiu rasmi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Joto ya Paris.

Paris ambao ni Mji Mkuu wa Ufaransa utakuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto kwa mara ya tatu Mwaka 2024, ambayo pia itaadhimisha miaka mia moja tangu michezo ya mwisho ya Olimpiki ifanyike Paris Mwaka 1924. Mji huo pia ulikuwa mji mwenyeji wa mashindano ya pili ya Michezo ya Olimpiki ya kisasa, Mwaka 1900.

Michezo hiyo imepangwa kufanyika kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11 huku Paris ikiwa mji mkuu mwenyeji. Viwanja vingine 16 vilivyoko Ufaransa na kimoja katika Eneo la Ng'ambo la Ufaransa la Tahiti pia vitaandaa mashindano wakati wa Michezo hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha