

Lugha Nyingine
Mchoraji picha wa Uganda atumia awapa mwanga wanafunzi alipowaelezea hali aliyojionea nchini China (2)
![]() |
Picha iliyopigwa Mei 8, 2018 ikionesha picha iliyochorwa na msanii Edward Kamugisha Ssajjabbi, picha hiyo ambayo ilioneshwa kwenye Maonesho ya Sanaa ya Kimataifa ya Beijing ya kila miaka miwili. (Xinhua) |
Katika picha aliyochora Edward Kamugisha Ssajjabbi ameeleza hadithi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya China wakati dunia ilipokabiliana na maambukizi ya UVIKO-19.
Hii ni picha moja aliyochora Ssajjabbi kwa kuonesha uhusiano kati ya China, Afrika na Dunia.
Ssajjabbi alizaliwa Kabale, eneo la vilimani la Kusini Magharibi mwa Uganda, na amepanda jukwaa la kimataifa kwa kupitia vipaji vyake na juhudi alizofanya bila kulegalega.
Wakati Ssajjabbi alipotembelea nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya sanaa, alialikwa kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya sanaa ya Beijing ya kila baada ya miaka miwili mnamo mwaka 2019, ambapo alikuja China kwa mara ya kwanza.
Alisema maonesho hayo ni muhimu sana kwa wasanii wa Afrika, kwa kuwa wanaweza kuonesha sanaa zao pamoja na wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani.
“Wasanii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani walishiriki kwenye maonesho hayo, ambapo wasanii wa Afrika wanafanya mabadilishano ya utamaduni na wasanii wa sehemu nyingine za dunia kwa kupitia mawasiliano ya kimaono,” alisema.
Baada ya kurudi nyumbani, Ssajjabbi alieleza hali aliyojionea nchini China kwa wanafunzi wake wa Chuo Kikuu cha Kabale.
Ssajjabbi anaona kuwa sanaa ni sehemu muhimu ya maendeleo ya kila nchi.
“Sanaa inatumika karibu katika kila sekta ya kila nchi kwa ajili ya kuhimiza maendeleo. Katika uhandisi, ukitaka kutengeneza unahitaji kuchora ramani ili kupata mwanga kwa usanifu rasmi. Hadi hivi sasa, bado haupo utamadauni wa aina yoyote usiohusiani na nguo, na hii ndiyo mitindo na usanifu ,” alisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma