Tukio la ufyatuaji risasi latokea katika uwanja wa ndege wa Love Field mkoani Texas, Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2022
Tukio la ufyatuaji risasi latokea katika uwanja wa ndege wa Love Field mkoani Texas, Marekani

Julai 25 kwa saa za huko, tukio la ufyatuaji risasi lilitokea katika uwanja wa ndege wa Love Field cha mji wa Dallas wa jimbo la Texas nchini Marekani, waokoaji walisema kuwa majeruhi mmoja alipelekwa kwenye hospitali, lakini utambulisho na hali yake ya kujeruhiwa hazijajulikana. Upande wa polisi ulisema kuwa tukio hilo la ufyatuaji risasi lilitokea karibu na kituo cha uuzaji wa tikiti. Watu waliokuwa kwenye foleni waliondolewa, njia za kutoka zilifungwa, na kwa sasa usafiri wa ndege zote katika uwanja huo ulisitishwa hadi saa 6:30 kwa saa za huko. Sasa tukio hilo linafanywa uchunguzi, na upande wa polisi haujapata habari nyingine zinazoweza kudokezwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha