Ufundi wa Juncao wa China waleta matumaini kwa wapandaji uyoga wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 27, 2022
Ufundi wa Juncao wa China waleta matumaini kwa wapandaji uyoga wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Picha iliyopigwa Juni 1, 2022 ikionesha uyoga uliopandwa na wataalamu wa China huko Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati. (Xinhua/Luo Yu)

Irene Dombeti wa Jamhuri ya Afrika ya Kati anaona yeye mwenyewe ni mmoja wa watu wachache wenye bahati ya kupata ufundi endelevu wa kupanda uyoga.

Alifanya utafiti juu ya ufundi wa kupanda uyoga wa chakula na uyoga wa matumizi ya tiba akitumia muda wa mwezi mmoja na nusu nchini China. Aliporudi Jamhuri ya Afrika ya Kati, aliona watu wa huko hawana hamu kubwa ya kutumia ufundi huo kupanda uyoga.

Baadaye wataalamu wa China walikuja nchi hiyo ili kufahamisha ufundi wa Juncao, yaani ufundi wa kupanda mmea unaoitwa “Juncao” wenye uwezo wa kuzoea hali ya mazingira, na mazao yake ni yenye virutubisho , na kutumia Juncao iliyofanyiwa utengenezaji zaidi kwa kupanda uyoga wa chakula na uyoga wa matumizi ya tiba, na kuwa chakula cha mifugo, alisema Chen Kehua, ambaye alileta mradi wa Juncao kwa Jumhuri ya Afrika ya Kati.

Bw. Chen aliandaa semina kwa mara 16 kutoa mafunzo juu ya ufundi wa Juncao, ambapo wanafunzi 613 walishiriki kwenye semina hizo, ambapo alifanikiwa kushirikisha ushirika 5 wa upandaji wa uyoga na ushirika 4 wa upandaji wa Juncao.

“Hivi sasa wameanza kuzoea kupanda uyoga baada ya kushuhudia tunayofanya, kwa sababu uyoga tunaopanda kwa ufundi wetu ni uyoga mtamu, na umevutia watu,” alisema Dombeti, ambaye hivi sasa ni fundi wa maabara ya Taasisi ya Kilimo ya China na Afrika.

Fatime Abba Rekya mwenye umri wa miaka 40 ni fundi mstadi wa kilimo na mfanya biashara wa uyoga, na pia ni mmoja wa watu waliovutiwa mapema zaidi na ufundi huo kutoka China.

Chini ya uungaji mkono wa wataalamu wa China, Abba Rekya alianza kutumia ufundi wa Juncao kupanda uyoga, na kuuza mazao kwenye mtandao wa intaneti.

“Hii ni biashara yenye matumaini makubwa, kwa sababu hapa kuna migahawa na hoteli, tunaweza kukausha uyoga na kuuuzia nchi za nje, na kufanya mambo mengi yanayohusika. Kwa vijana wasiopata elimu, tunaweza kuongeza nafasi za ajira kwao, na vilevile kwa wanawake wanaokaa nyumbani,” aliongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha