Xi akabidhi nishani ya Agosti Mosi kwa wanajeshi mashuhuri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2022
Xi akabidhi nishani ya Agosti Mosi kwa wanajeshi mashuhuri
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akiwa katika picha ya pamoja na waliopokea nishani ya Agosti Mosi mjini Beijing, China, Julai 27, 2022. Jumatano wiki hii Rais Xi alikabidhi nishani ya Agosti Mosi kwa wanajeshi watatu na kukabidhi bendera ya heshima kwa kikosi cha kijeshi kwa utumishi wao uliotukuka kabla ya maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA). (Xinhua/Li Genge)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatano wiki hii alikabidhi nishani ya Agosti Mosi kwa wanajeshi watatu na kukabidhi bendera ya heshima kwa kikosi cha kijeshi kwa utumishi wao uliotukuka kabla ya maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China. (PLA).

Rais Xi, aliwasaidia watu hao kuvaa nishani zao, kuwakabidhi vyeti vya heshima, na kupiga nao picha.

Pia alitunuku bendera ya heshima ya kuheshimu mchango wa kikosi cha mfano cha makombora ya ardhini hadi angani cha Jeshi la Anga la PLA.

Xu Qiliang, Naibu Mwenyekiti wa CMC, alisoma maagizo yaliyotiwa saini na Rais Xi ya kuwapa heshima wanajeshi na kikosi hicho. Hafla ya kukabidhi tuzo hiyo iliyofanyika Beijing, China iliongozwa na Zhang Youxia, ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa CMC.

Maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa PLA yatafanyika Agosti Mosi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha