Rais Xi Jinping asisitiza kudumisha ujamaa wenye umaalumu wa China ili kujenga nchi ya kijamaa yenye mambo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2022
Rais Xi Jinping asisitiza kudumisha ujamaa wenye umaalumu wa China ili kujenga nchi ya kijamaa yenye mambo ya kisasa
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, akitoa hotuba muhimu kwenye ufunguzi wa kikao cha mafunzo kwa maafisa wa ngazi ya mkoa na wizara. Kikao hicho cha masomo kimefanyika kwa siku mbili za Jumanne na Jumatano hapa Beijing, Mji Mkuu wa China. (Xinhua/Ju Peng)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kushikilia juu bendera ya ujamaa wenye umaalumu wa China na kujitahidi kuandika ukurasa mpya kabisa katika kujenga nchi ya kijamaa ya kisasa katika mambo yote.

Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, ametoa kauli hiyo kwenye ufunguzi wa kikao cha mafunzo kwa maafisa wa ngazi ya mkoa na wizara kilichofanyika kuanzia Jumanne hadi Jumatano mjini Beijing, China.

Xi amesisitiza kufuata ujamaa wenye umaalumu wa China na mwongozo wa mafanikio ya hivi karibuni katika kuufanya U-Marxi uendane na mazingira ya China na mahitaji ya nyakati katika safari mpya ya kujenga nchi ya kijamaa ya kisasa katika mambo yote.

Amesisitiza kuimarisha imani katika njia, nadharia, mfumo na utamaduni wa ujamaa wenye umaalumu wa China na kuendeleza mchakato wa kihistoria wa ustawishaji wa Taifa la China.

Ufunguzi wa kikao hicho ulihudhuriwa na Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji na Han Zheng, ambao wote ni wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC. Makamu wa Rais Wang Qishan pia alihudhuria.

Akielezea umuhimu wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC utakaofanyika katika kipindi muhimu kwenye safari mpya ya kujenga nchi ya kijamaa yenye mambo ya kisasa katika mambo yote, Xi amesema malengo, kazi na sera kwa ajili ya CPC na nchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo na kuendelea itafanywa kwenye mkutano mkuu huo.

“Ni muhimu sana kujenga juu ya mafanikio yaliyopita ili kuendeleza zaidi malengo ya Chama na nchi, kwa mustakabali wa ujamaa wenye umaalumu wa China, na kwa ustawishaji mkubwa wa Taifa la China.” Xi amesema.

Amesema, kutokana na hali ya mwenendo wa mabadiliko ya kimataifa ambayo hayajawahi kuonekana katika karne hii, na hatari ngumu zaidi, changamoto, ukinzani na matatizo, “kazi ya msingi ni kuendesha vizuri mambo yetu wenyewe.”

Amesema, miaka mitano iliyopita tangu Mkutano Mkuu wa 19 wa CPC imekuwa ni yasiyo ya kawaida.

“Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China imeunganisha na kukiongoza Chama kizima, jeshi, na watu wa China katika kukabiliana vilivyo na hali mbaya na tata ya kimataifa na mlolongo wa hatari na changamoto kali, na kuhimiza ujamaa wenye umaalumu wa China uendelee katika zama mpya.” Xi amesema.

Xi amesema, China imelinda kwa uthabiti usalama wa taifa, kudumisha utulivu wa jumla wa kijamii, kusukuma mbele ulinzi na uboreshaji wa jeshi, kulinda kwa uthabiti amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan, na kuhimiza diplomasia ya juu ya nchi kubwa yenye umaalumu wa China katika sekta zote.

Maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China yalifanyika katika kipindi hicho, na CPC iliadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na kuanzisha kampeni ya kujifunza historia ya CPC.

Xi pia ametaja mafanikio katika mapambano dhidi ya UVIKO-19, kutunga Sheria ya Kulinda Usalama wa Taifa katika Eneo la Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, kusimamia na kuratibu vema usimamizi wa mikoa ya China yenye kujiendesha au ya utawala maalumu hususani Xinjiang na Tibet na kuhimiza nidhamu na uadilifu.

Xi ametoa wito wa kufanya maamuzi ili kushiriki kikamilifu kwenye mapambano makubwa na vipengele vingi vipya vya mambo ya kisasa, na utayari wa kufanya kazi kwa bidii zaidi kuelekea lengo la ustawishaji wa Taifa la China.

Amesema, mafanikio yote katika miaka 10 iliyopita yalifanywa kutokana na juhudi za pamoja za CPC na wananchi.  

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha