Benki Kuu ya Zimbabwe yatambulisha sarafu za dhahabu kama hifadhi ya thamani huku kukiwa na mfumuko mkubwa wa bei

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2022
Benki Kuu ya Zimbabwe yatambulisha sarafu za dhahabu kama hifadhi ya thamani huku kukiwa na mfumuko mkubwa wa bei
Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mangudya akionyesha sarafu mpya ya dhahabu kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, Zimbabwe, Julai 25, 2022. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)

HARARE - Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mangudya Jumatatu wiki hii alitambulisha sarafu mpya za dhahabu ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika kama hifadhi ya thamani na kupunguza mahitaji ya dola za Marekani wakati nchi hiyo ikipambana kudhibiti mfumuko wa bei unaoongezeka.

"Benki hii leo imeingiza sokoni kundi la kwanza la sarafu 2,000 za dhahabu za Mosi-oa-Tunya (Moshi unaovuma). Mashirika ya ndani yalianza kuuza sarafu hizo za dhahabu kwa misingi ya uwakala kwa bei ya awali ya dola za Kimarekani 1,823.83 kwa kila sarafu ya dhahabu au dola za Zimbabwe 805,745.35 kwa kutumia viwango vya bei vinavyokubaliwa na mnunuzi na muuzaji vya Ijumaa (wiki iliyopita)," Mangudya amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Harare, mji mkuu wa Zimbabwe.

Miongoni mwa sifa nyingine, sarafu hiyo ya dhahabu itakuwa na thamani ya ukwasi wa mali, thamani ya mali iliyowekwa, inaweza kutumika kama dhamana, kuuzwa na kununuliwa kwa idhini ya mmiliki.

Watu binafsi, makampuni ya ndani ikiwa ni pamoja na wawekezaji wa kitaasisi wataruhusiwa kununua sarafu hizo za dhahabu kwa fedha za ndani pamoja na fedha za kigeni, wakati wanunuzi wa kimataifa watanunua tu sarafu hizo kwa fedha za kigeni ambazo ni pamoja na dola ya Marekani, Randi ya Afrika Kusini na Pauni ya Uingereza miongoni mwa nyinginezo.

Bei ya sarafu inategemea bei ya kimataifa ya dhahabu pamoja na asilimia 5 ili kufidia gharama ya uzalishaji na usambazaji wa sarafu kwa malipo dhidi ya utoaji.

"Sarafu za dhahabu kama tulivyoshauri hapo awali, ni bidhaa mbadala nzuri ya uwekezaji kwa wale wanaotaka kuhifadhi thamani. Dhahabu ni mali ya akiba iliyo salama na ya kutegemeka duniani kote," amesema Mangudya.

Pia amesema wanunuzi binafsi na wa kitaasisi wanatakiwa kushikilia sarafu hizo kwa angalau siku 180 kabla ya kuziuza, na kuongeza kuwa mauzo yote yatakuwa chini ya Mfahamu Mteja Wako na wanunuzi wanatakiwa kutangaza chanzo cha fedha zao.

Kuanzishwa kwa sarafu hizo za dhahabu ni sehemu ya hatua za Serikali ya Zimbabwe za kukabiliana na mgogoro wa sarafu ya nchi hiyo ambao umepelekea dola ya ndani kushuka kwa kasi.

"Tunachotarajia kuona ni kwamba tunashuhudia utulivu katika kiwango cha ubadilishaji na kwahivyo kwa kuongeza athari za kupita kwenye mfumo wa bei, viwango vyote vitashuka. Kwa hivyo tunatarajia kuona utulivu wa bei katika uchumi," Mangudya amesema.

Kufuatia miaka mingi ya mfumuko mkubwa wa bei, Zimbabwe iliachana na sarafu yake ya dola Mwaka 2009, na kuamua kutumia fedha za kigeni, hasa dola ya Marekani.

Serikali ilirejesha sarafu ya ndani Mwaka 2019, lakini imepoteza thamani kwa haraka, na hivyo kurudisha kumbukumbu za kipindi cha mfumuko wa bei ambao ulipunguza akiba za watu wengi. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha